Jiajiri

Ben40

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2012
Posts
207
Reaction score
37
Ni biashara gani naweza kufanya kwa mtaji wa elfu hamsini wana jf?
 
Mkuu huo ia mtaji ni mkubwa sana na inategemea unataka kufanya vitu gani

- Labuda ungekuja na unacho penda kukifanya ndo tukushauri ila kwa biashara inatosha kabisa, ila njoo na mawazo yako hata matano then watu humu watakusaidia kuchambua
 
Unaweza Biashara ya kuuza Chapati.

Nenda kaulize haya.

Bei ya ngano 1kg.
1kg inatoa chapati ngapi?
Chapati moja ni Bei gani?
Chukua tenda ya kupeleka vitafunwa maofisini asubuhi.

Najua utadharau lakini kwa mtaji wako biashara utakayofanya lazima ufanane na hii.
 
Zaidi ya mtaji ungejieleza, kazi yako au unaishi wapi na hata uliipataje ingesaidia mtu akuelekeze ufanye nini
eti Vivian, wanaume nao wanapika chapati tena?
funguka zaidi, kuna vitu mtu wa jinsia hii anaweza kufanya vizuri tu wkati kwa jinsia nyingine itakuwa ngumu,
pia kuna wanafunzi wanakaa na hawana muda wa kupika, wakati mtu wa ofisini anaweza usiku kupika hiyo chapati na asubuhi akawauzia staff wenzie... mwanafunzi anaweza kuchagua mitumba mizuri na kuiuza kwenye hostel ila mtu mgeni wakimkopa watakimbia kulipa, idea ziko nyingi ila uwe wazi zaidi
 
Nataka kufuga kuku au nguruwe na nimgeni katika ufugaji je nifanyeje wana jf?
 

ngano kg inauzwa 1300 Tshs.
 
Sio kweli kuuliza si ujinga bujibuji.
 
Nataka kufuga kuku au nguruwe na nimgeni katika ufugaji je nifanyeje wana jf?
ni kweli nguruwe au kuku wa kienyeji wanaweza fugwa kwa unafuu sana kwa kuwalisha vyakula vinavyobaki nyumbani au shambani,
lakini sina uhakika na nguruwe hata wale wadogo wanauzwa sh ngapi siku hizi, ungeweza nunua wawili ukaanzia nao
kuku kama ni wa kienyeji unaweza kupata hata wanne au watano kutegemea na unaishi wapi kisha kama una eneo lako ukafanya zero grazing
tafadhali tafuta threads za kuku hapa ujasiriamali ni nyingi tu utapata ujuzi mwingi jinsi ya kufanya hii biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…