SoC03 Jiamini, mtazamo wa kijana

SoC03 Jiamini, mtazamo wa kijana

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Jun 1, 2023
Posts
1
Reaction score
1
MALENGO ni kuweza kuonyesha unapo JIAMINI unaweza fanya jambo kubwa kuwa dogo na dogo kuwa kubwa .Kama utafuata misingi bora yenye kanuni nzuri zenye tija endelevu katika jamii husika..
Kwa kutumia misingi bora tunaweza kuanzisha vikundi vya kutetea maslahi ya kijinsia na kukuza maendeleo katika jamii husika

CHANGAMITO KUWA FURSA ni kuangalia matatizo yaliyopo kwenye jamii iliyopo katika mtizamo chanya ili ziwezekuwa chachu ya maendeleo na kujikwamua kimaendeleo na kujenga jamii mpya yenye mtizamo mzuri wenye faida katika jamii husika.

Changamoto zipo nyingi kwa mtazamo wangu Mimi ni kama ifuatavyo -
a) Zinazooneka (b)Zinazohisiwa (c)Miundo ya familia na Jamii husika (d)Makampuni ya kifedha

Nitaelezea kwa ujumla KUSUBUTU AU KUJARIBU( MBEGU) hii ndio sehemu au kipindi kigumu sana katika maendeleo jamii husika.Hii hali mda mwingine mwingine hupelekea kupungua uwezo wa kujiamini ambao ndio msingi mkubwa wa maamuzi ya KUSUBUTU au KUJARIBU.

Katika kipindi hichi kunaitajika elimu au uelewa ambao ndio chachu au chungu ya maendeleo na mafanikio.Elimu inahitaji vitu vingi sana iwebora na iwe na tija katika jamii, elimu bila manufaa ni kama nyumba nzuri isiyo tumika lazima ichakae tu kwa asili pia.Elimu bora ni lazima iwe na manufaa katika jamii husika na elimu sio eti kusoma sana kupata vyeti vingi vikubwa na vidogo laasha,Elimu ni kuwa na uelewa wa kuamua na kufanya maamudhi chanya katika kufanya jambo ambalo ni tofauti na mwingine katika jamii husika.

Elimu inapotumika vizuri kwajua na kutoa unaloelewa katika jamii naweza sema kufanya mgawanyiko wa elimu kwa wanajamii bila kubagua. Na ndio maana wahenga husema ELIMU NI BAHARI.Kwa maana kuwa uwezi jua kila jambo katika ulimwengu au jamii ,hivyo basi kutokana hali hii kunaitajika mgawanyiko wa elimu na watu wanaokuzunguka ili kujua changamoto na mitazamo yao katika fikra mbalimbali.

Elimu ni chachu sana katika kujiamini ili kujenga jamii bora na sio bora jamii,Elimuili yenye manufaa ni muhimu sana na sio yakutaka kutawa jamii kwa vingezo kuwa unatakuwa kiongozi.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya KIONGOZI NA MTAWALA, KUONGOZA NA KUTAWALA asili mia kubwa wenye elimu hutaka kutawala na sio KUONGOZA elimu ina mlango mpana sana tofauti kati ya kiongoza na mtawwala kama ifuatavyo;

KIONGOZI
(A)Hupenda kusikiliza maoni na mawazo
(B)Hatamani madaraka sana
(C)Mpole na mwenye huruma na unyenyekevu
(D)Huwa mwenye subira ya maamuzi
(E)Hupenda sana kujua madhaifu na mapungufu yake na Jamii yake pia kwa maendeleo ya wote.
Lakini MTAWALA huwa kinyume na hayo yeye hufanya kwa masilai yake binafsi.


Nahizo ni miongoni mwa tofauti kati ya MTAWALA na KIONGOZI

DHUMUNI ni kila mwanajamii anajitajika kujiamini kuwa anaweza fanya jambo jema lenye tija kati jamii pia akumbuke kuna kundi la watu linamtengemea katika jamii yake kwa uwezo aliokuwa nao.Kuna makundi muhimu sana Tena sana ambayo ni VIJANA NA WAKINAMAMA,Kwa sababu makundi haya ni muhimu na ndio msingi wa Taifa na wa kila jambo pia.Haswa WAKINAMAMA Kwa sababu wa ndio walezi wa makundi yote ya kijinsia.Mama nikama shina katika familia au kiungo wa mawssiliano kati ya baba na watoto ambapo ndipo chanzo Cha Taifa.

PENDEKEZO ni VIJANA tukutumika vizuri tunaweza kuzui au kutokomeza yafuatayo Uharifu,Mimba za utotoni,Utoloshuleni,Ajali za barabarani na Ujinga pia umasikini.
Kwa kudumisha UPENDI wenye zao la AMANI.

NINI KIFANYIKE ni kushirikisha vijana katika kujadili na kupokea mitazamo bila kubagua uchumi au elimu ya mtu pia vijana wengi wanakuwa wanaogopa kujiweka wazi katika kufanya maendeleo ya jamii kwa kuofia kuwa hawa Elimu ya mashuleni.Na hivyo hupelekea vijana wengi kuto kujishuulisha kwa kuwa wanyanyapaliwa katika mawazo .Hupelekea pia kushindwa ata kufuatilia haki zao pia ,hivyo basi husababisha vijana wengi kujiunga katika makundi mabovu ya Uharifu nk.

Kupitia andiko au sera hii itamfanya kijana AJIHAMINI na KUSUBUTU kufanya baadhi ya mambo au kutatua changamoto.

Pia kuwepo na mikopo yenye riba nafuu na mashariti nafuu na Miata elimu ya mikopo husika ambayo wengi hawana nahivyo kupelekea vijana kuweza kusubutu ata akisubutu huanguaka.

Ikifuata taratibu za kujali vijana itafanya vijana kuto kufa na MALENGO yao.

Semina ziwepo za wazi kati vijiji ,kata na ata wilaya na vijana wachangue wenyewe wakilishi wao na sio kuchanguli na kuandaliwa kwa masilahi ya wengine.

Vijana tuandaliwe kifikra na mitazamo mizuri ya kuwa Mimi au sisi ndio walezi wa Taifa na Familia zetu na kuwa uzalendo ni jukumu letu kwa pamoja kwa kusimamia maslahi ya Kila mwajamii katika nafasi yake na kuwepo mirejesho Kila wakati katika jamii amabayo itasaidia kujua tunatoka wapi tunaenda wapi.

TUJIAMINI TUNAWEZA NA KWA KUWA SHIDA SI SHIDA BALI SHIDA NI MTAZAMO WA SHIDA YENYEWE

SHUKRANI KWA MUNGU ,JAMII FORM NA FAMILIA
 
Upvote 1
Back
Top Bottom