ASIWAJU
JF-Expert Member
- Nov 18, 2022
- 1,938
- 1,632
Aliyekuwa Rais wa China bwana Jiang Zemin amefariki dunia leo alfajiri mjini Shanghai China akiwa na umri wa miaka 96.
Taarifa kutoka vyombo vya utawala vya China [ kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China, kamati ya kudumu ya bunge la taifa la China , Baraza la mashauriano ya kisiasa na kamati kuu ya kijeshi] zinasema bwana Jiang Zemin ameaga dunia kutokana na saratani ya damu na kushindwa kwa viungo vya mwili, baada ya matibabu yote kushindikana. kwenye barua iliyo andikwa kuutarifu umma wa China kuhusu kifo hicho.
Komredi Jiang Zemin ametajwa kuwa alikuwa kiongozi bora aliye heshimiwa na Chama kizima,jeshi lote na watu wa China wa makabila yote, mfuata nadharia ya u-marxist mkuu mwanamapinduzi mkuu wa tabaka la wafanyakazi, mtawala mwana mikakati ya kijeshi na mwanadiplomasia, mpiganaji wa muda mrefu wa ukomunisti aliyepata changamoto na kiongozi mahiri aliye pigania ujamaa wenye umaarufu wa China.
Pia ametajwa kuwa alikuwa nguzo ya uongozi wa pamoja wa kizazi cha tatu Cha chama cha kikomunisti cha China, na mwanzilishi mkuu wa nadhari ya uwakilishi mtatu.
Chanzo: CRI Swahili.