Nafikiri sasa ni wakati wa kufikiri nje ya Box. Unaona Microfinance nyingi, Blue Finance, Mwananchi, Opportunity etc. Umewahi jiuliza pesa wanazokopesha wanazitoa wapi?, Je ni kwasababu hujui walizozipata?
Je, Unapo deposit pesa zako Bank ( Be it NBC, SCB, Twiga, NMB) huwa security ni nini?. Naelewa nad nakubali tunajadili ili mwisho wa siku tujenge na tujenge kilicho bora kwa maslahi ya Watanzania walio wengi.
Pyramid Scheme. Kwa ufahamu wangu na mapokeo yangu ya mfumo huu ni kuwa, Mwisho wa siku wengi hukosa faida kutokana na wenda kutopata pesa za wachangiaji wapya.
Maana hii naamini si sahihi kwa mfumo ambao JIBU wanautumia kutimiza malengo yao, ambayo moja wapo ni kurahiisha upatikanaji wa pesa kwa wahitaji. Wao JIBU hukopesha kwa masharti yaliyo wazi na kwa riba, yaani ukikopa utarudisha kwa kiasi fulani chariba juu ya principal. Na vivyo hivyo ukiikopesha hii Kampuni wao watakulipa riba juu ya Principal uliyo wakopesha. Tofauti ya riba wanayotoza their borrower na riba wanayomlipa lennder wao ndio faida. Je Pyramid hapa iko wapi?
I stand to be corrected. Kwa mfumo wa Jibu, hakika ni mkombozi kwa wale wenye pesa and hawana mifumo rahisi ya kuwekeza, bila gharama kubwa za uendeshaji. Lakini pia kwa baadhi ya wengi ni mwiba hasa kwa ma Bank na taasisi zingine ambazo zinanyonya wateja kwa deposit interests ndogo sana kwani kuna hatari wateja wakakimbia.
Karibu tujadili kwa mapana zaidi.
Happy Easter Monday