Tuliwahi kupost habari ya hii kampuni kuja mjini Arusha na kufanya kazi kama DESI. Chanzo cha habari toka maeneo ya Kijenge makao makuu ya hii kampuni ni kwamba inadaiwa na zaidi ya wateja wake 300 na haionyeshi dalili za kulipa madeni.
Watanzania kwa kupenda dezo!!!hatujambo yaani unaona kabisa anayekuambia atakupa pesa shida zimemzonga mpaka uvunguni lakini bado unampelekea pesa ili akuzalishie.Ina maana upatu,dollar jet,DECI haikua fundisho tosha kwa wananchi?