Ninachosikitika siasa zimetugawa, yaani imekuwa kama uadui, na hii sumu wanaisambaza watu wa upinzani ni sumu mbaya sana, itafika kipindi utashindwa kumsaidia mtu tu kisa itikadi zenu tofauti, sasa kosa la diamond platnumz lipo wapi, hii inchi kila mtu yupo free kuchagua anachokitaka ili mradi asivunje sheria, diamond kawasilisha maoni yake kupitia mziki. Kuwa na itikadi tofauti isiwe tatizo, ila Ninachosikitika sana wanasiasa na mitandao ya kijamii inatugawa vibaya sana, mpaka inafikia Kipindi tunaomba mabaya yatokee kwa nchi yetu, ili kuikomoa serikali, yaani mpaka kwenye kusifia tunakosoa na kwenye kukosoa tunasifia.Watu wanaomponda diamond platnumz ndio hao wanalalamika kila siku inchi haina demokrasia, lkn hawajui diamond platnumz ametumia haki yake ya msingi ya demokrasia kawasilisha mawazo yake kupitia mziki wake. Tanzania kwanza, tusilichukulie hili swala la ROMA kisiasa eti ni la upande fulani. Nammlaani sana kimambi, kwani hii sumu anayoisambaza, haina tofauti na kile kituo cha radio Rwanda kilichorusha habari za kibaguzi, mwisho wake kukawa na mauwaji ya Kimbari. Watanzania tuwe makini sana tusiruhusu mitandao ya jamii na wanasiasa watugawe.