Jicho la Tatu: Upo uwezekano Rais anashauriwa vibaya

Jamaa punguza malalamiko.....fanya kazi usitegemee Rais akupe hela.

😂😂
 
Tatizo nchi hii hakuna aliye msafi, kila mtu mwizi. Akipata upenyo tu anakwapua Kwa nguvu au kalamu.

Yaani watu wote ni wa deal deal tu. Na ndio tulivyokuzwa kutokujemimea maovu kisa tutaharibia watu na sisi tusije haribiwa nafasi ikipatikana.
Tena ukiwa mwadilifu hata ofsini unaitwa una roho mbaya na watu wanakutangaza kabisa kwamba wewe ni mtu wa hovyo.

Miafrika kwa wizi ni pete na kidole
 
Hakuna anayemharibia maana kila mtu anafata maelekezo yake. Kwa hiyo mazuri na mabaya ni juu yake mwenyewe.
 
Nukuu kutoka kitabuni.

"Ninakuruhusuni kunishauri chochote mnachoweza kunishauri, iwe hoja chanya na mathubuti au hoja zisizo kuwa na afya.

Siyo lazima nifanyie kazi chochote mtakachonishauri, hiyo inabaki juu yangu na akili yangu"

Karist Mjuni, kwenye kitabu cha MITIHANI kiliandikwa na George Iron Msoenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungetulia uandike Taratibi kwa Aya labda ungetoa hoja nzuri zaidi..Nashauri anzisha uzi mpya uandike vizuri tuelewe
 
Sio kushauriwa vibaya, bali ana uwezo mdogo kiakili
 
Rais hatakiwi kuwezekana kushauriwa vibaya.

Rais akishauriwa vibaya, na kuukubali ishauri huo, hilo ni kosa lake.

Kwa sababu, kwanza hao washauri anawateua mwenyewe, ana nguvu ya kuwateua na kuwatengua muda wowote, bila hata kutoa sababu.

Pili, urais ni taasisi yenye resources nyingi sana za kupima mashauri kabla ya kuyakubali. Rais halazimiki kukubali ushauri, na akiukubali ushauri mbaya, mambo yakaharibika, lawama za mwisho zinaenda kwa rais.

Wakati wa urais wa Nyerere, washauri wake rasmi wa uchumi walimwambia ataifishe maduka yote nchini. Mpaka maduka ya mitaani ya Waswahili wa kawaida.Nyerere aliuchukua ushauri huu wa washauri wake wasomi, kabla ya kuukubali, Nyerere akasema ni muhimu afanye kitu kinaitwa "ushirikishwaji wa umma", akasema nitaupima ushauri huu unakubalika vipi na watu wa kawaida.

Nyerere alikuwa ana wahauri wengi rasmi, lakini oia alikuwa anajuana na wazee wengi wa Dar es salaam. Wazee tu wa chama. Akamuita M,ee mmoja anaitwa Tabu Mangala. Mzee Tabu Mangala alikuwa Mzee tu wa Kiswahili, kiongozi wa Yanga.

Nyerere akamuuliza Tabu Mangala, akamwambia, nimeshauriwa kutaifisha maduka yote, mpaka madogo ya mtaani. Unaonaje jambo hili, litafaa?

Mzee Tabu Mangala akamwambia Nyerere jambo hilo halitafaa chonde chonde Baba usifanye hivyo, huko Uswahilini wenyewe tunajua tunavyositiriana si sawa kutaifisha maduka yote.

Nyerere akamsikikiza Tanu Mangala, akauacha ushauri wa wasomi wake.

Habari hii imeandikwa katika kitabu, nafikiri cha tatu, katika series ya "Development as Rebellion: A Biography of Julius Nyerere" iliyoandikwa na Issa G. Shivji, Ng'wanza Kamata, na Saida Yahya-Othman.

Rais wa Marekani Harry S Truman alikuwa anafanya ziara kwenye gereza moja la serikali huko Oklahoma. Gereza lilikuwa kubwa sana, lina mashamba na karakana na vitu vingi. Alivyomtembelea mkuu wa gereza, akakuta kwenye meza ya mkuu wa gerwza pameandika "The Buck Stops Here".

Akamuuliza yule mkuu wa gereza, kwa nini hapa umeandika hivi "The Buck Stops Here"? Yule mkuu wa gerwza akajibu kwamba, hili gereza kubwa sana, lina wafanyakazi wengi. Kila siku kitu kikiharibika, nikiukiza napewa story nyingi, kila mtu anamlaumu mwingine, kila mtu ni kama ana kindoo fulani cha lawama anakitupa kwa mwingine , lakini hicho kindoo cha lawama, ultimately kinaishia kwangu. So, the buck stops here. Lawama zote zinaishia kwangu.

Rais Truman aliupenda sana huo msemo, akaagiza achongewe kibao chenye msemo huo na kukiweka kwenye meza yake Ikulu ya Marekani.

Noblesse oblige, aliyepewa cheo kikubwa zaidi, atadaiwa zaidi, aliyepewa talanta zaidi, atadaiwa zaidi.

Rais akipewa ushauri mbaya, akaukubali, lawama zinaenda kwa rais. Rais ndiye mwenye makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…