Jicho la tatu

Jicho la tatu

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
FB_IMG_1724852336811.jpg

Imeandaliwa na kuandikwa na Dokta Dotto Aliko

🗣️Tuna macho mawili ambayo Ni macho ya uongo fake eyes, lakini pia tuna jicho moja ambalo ndiyo jicho la kweli true eyes, Hivyo tuna macho matatu lakini mawili Ni ya uongo na moja Ni la ukweli nalo siyo lingine Ila Ni lile lililopo Kati Kati yaa paji la uso.

👁️Iangalie Nazi moja Kati ya bidhaa ambayo inamaajabu sana, siko hapa kuzungumzia maajabu ya Nazi Ila Nazi Ni mfano mzuri wa hiki ninachokizungumza hapa Nazi Ina macho matatu, Kati yao mawili ya uongo na moja Ni lakweli.

✍️Jaribu kuangalia vile vitobo vitatu vya Nazi, Ni kimoja tu ndiyo ukikitoboa kinatoboka na kutoa maji Ila vile viwili Ni mfano tu wa kitobo Ila siyo vitobo, Basi ndiyo mfano wa haya macho yetu ya kifizikia na jicho la tatu.

👀Haya macho yetu Ni macho ya uongo, Kama ulivyo huu mwili wa uongo ndivyo yalivyo macho yetu, Ila Kuna jicho la kweli ambalo Ni moja tu.

👁️Nalo siyo lingine Ila Ni lile jicho ambalo lipo katika paji la uso, jicho la tatu, Hili ndiyo jicho lenye uwezo wa kukuoneshea Yale usiyoyaona.

🗣️Rejea Ile stori ya yesu anawaponya vipofu wawili bado Ni fumbo Hili hili la macho ya uongo na jicho la tatu, Wale vipofu wawili Ni macho yetu haya mawili ya kifizikia ambayo hayawezi kuona Yale Mambo ya kiroho, lakini yesu anawafunga macho yao kwa mikono yake na baada ya kuwaachia nao wanasema kwamba wanaona. Hapa Kuna SoMo lingine ambalo mnatakiwa muelewe kwamba ili tuone ya kiroho Basi milango ya kifizikia inatakiwa ifungwe.

✍️"Jicho ni taa ya mwili. Kama basi jicho lako ni zima, mwili wako wote utakuwa katika mwanga." Unafikili kwa Nini hapa imetumika jicho na Wala siyo macho kwa sababu haya macho mawili Ni macho ya uongo Ila jicho la kweli Ni moja.

🤔Wazee wetu walikuwa wanawapaka wanja watoto wadogo kwenye paji la uso, kwa Nini wawapake kwenye paji la uso na Wala so sehemu nyingine, wazee wetu wanajua Nini walikuwa wanafanya na walikuwa wanafanya hivyo kwa ajili ya kumkinga mtoto na tatizo la kushtuka shtuka, je kwanini mtoto anashtuka shtuka Ni kwa sababu jicho lake la tatu liko wazi anayaona yake ambayo hayaonwi kwa macho ya kawaida Sasa akipakwa majibu au wanja inafunga jicho la tatu na kumfanya mtoto asione vitu vya kiroho na aache kushtuka shtuka.

👌Rejea siku ya jumatano ya majivu, je Yale majivu yanapakwa wapi, kwenye paji la uso, na kauli mbiu yake Ni kwamba wewe Ni mavumbi naa mavumbini utarudi, yaani unatolewa katika ukiroho na kuletwa katika Hali ya kifizikia huku nawe ukiamini kwamba kweli wewe Ni mavumbi kumbe si mavumbi wewe.

✍️ Mwalimu wako Dotto Aliko
 
Kama wazee walipaka watoto wanja kuziba jicho la tatu na jumatano ya majivu wanapaka kuziba nini?
 
Back
Top Bottom