Jicho langu katika teuzi za Viongozi

Jicho langu katika teuzi za Viongozi

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Huko miaka ya nyuma viongozi walikuwa wanachaguliwa kutokana na mafunzo ya uongozi waliyo yapata kutoka katika vyuo husika,,mfano husika ni kile Chuo cha CCM Kivukoni.

Huko viongozi walikuwa wanapikwa na kuiva haswa na kuwa tayari kuihudumia jamii,walikuwa wamelelewa katika maadili ya uongozi

Haikuwa raisi kuona viongozi wanao ropoka hovyo majukwaani,haikuwa raisi kuwaona viongozi wanao dhalilisha walio chini yao kisa tu wao wana vyeo vya juu,,hakukuwa na viongozi ambao wanatafuta kiki mitandaoni kwa gharama ya kuwa dhalilisha watu wengine.

Na bahati mbaya zaidi wananchi wanadhani viongozi bora ni wale wanaoropa majukwaani na kuwakalipia watu bila sababu za msingi,,huo sio uongozi bora.

Kiongozi ni yule anaye onyesha njia sahihi ya kupita kwa walio chini yake wamfuate,na hata pale inapotokea wafuasi wake wakakosea basi huwa elekeza katika namna ambayo wataielewa vizuri na kuongeza mshikimano katika utendaji wao

Si maanishi kwamba kiongozi asiwe mkali la hasha! Katika misingi ya uongozi kuna wakati kiongozi anatakiwa awe mkali kama Chui,,lakini hii huwa ni mara chache sana hasa pale baada ya njia zote za busara na hekima kushindikana,,na kiongozi akifikia hatua hiyo hata huyu mkosefu anajua kweli hapa nimeyatimba.

Natumaini wote tutakubaliana enzi za marehemu Benjamini Mkapa katika uongozi wake alifanya teuzi zake kwa kufuata misingi ya uongozi,na ndio maana ilikuwa vigumu kukutana na viongozi wenye kutafuta kiki kama ambao tunao leo,hakukuwa na viongozi wenye kutafuta umaarufu kwa kuwadharau wengine au kuwadhalilisha wengine

Lakini mambo yalibadilika katika awamu zilizo fuata baada ya teuzi kufanywa kwa kuangali umaarufu wa mtu au kwa kujuana au kwa kuteua watu hata kama hawana fani ya uongozi

Tulishuhudia watangazaji wanakuwa wakuu wa wilaya,warembo wanashika nafasi za uongozi na wanamuziki wanashika nyadhifa mbali mbali.

Ieleweka vizuri hapa,sipingi watu hawa kuteuliwa na kushika nafasi mbali mbali za uongozi,kwani baadhi yao wameonyesha dira nzuri katika uongozi wao,mfano Betty Mkwasa, Niki wa Pili,Mwana FA, Abdallah Mwaipaya,Fatuma Almasi na mlimbwende Jokate Mwegelo

Hao na wengine wameonyesha nidhamu nzuri ya uongozi,,lakini pamoja na hayo kuna haja kubwa sana viongozi kupewa semina fupi fupi juu ya fani ya uongozi mara kwa mara ili kuwawezesha kuwa katika misingi bora kabisa

Kinyume chake leo hii kuna viongozi wanatoa kauli mpaka unajiuliza hivi huyu ni kiongozi kweli au ni kiongozi wa mchongo,halafu unajiuliza tena hivi aliye mteua kiongozi naye anajua anacho kifanya kweli?

Maana mwisho wa siku viongozi hawa wabovu wanamtukanisha aliye wateua,,maana tunajiuliza je kabla hawajateuliwa haukufanyika mchakato mzuri wa kumteua mtu huyu? Je hii aibu tunayopata leo hawa wateuzi wake hawakuiona mapema .

Maana sifa moja wapo ya kiongozi ni kuwa na maono ya mbele, sasa kama wateuzi hawaoni mbele basi si ajabu wakateua watu ambao sio sahihi kabisa.

Napenda kutoa ushauri wa bure kwa wateule dunia imebadilika sana,watu wanapata taarifa kwa njia rahisi mno,kwahiyo matendo yako ima yatakunyanyua au kukuangusha,ima yatakuongezea thamani au kushusha thamani yako.

Muache huu upuuzi wa kutaka umaarufu kwa kutrend mitandaoni, ni watu wapuuzi tu ndio watawaona mna maana lakini wenye busara na hekima zao wanaona ni wapuuzi

Kuna watanzania wengine hawakupata nafasi ambazo mmepata nyinyi basi zitendeeni haki,onyesheni kweli hamkuchaguliwa kwa bahati mbaya bali mlistahili nafasi hizo

Na mwisho matendo yenu ima yatamvua nguo aliye wateua au kumuheshimisha,kwahiyo mna dhima kubwa kumuheshimisha huyo aliye waamini na kuwapa madaraka na sio kinyume chake.

Ni hayo tu!
 
Uongozi una misingi yake...

Hawa viongozi wa kisiasa wana tabia ya kuwaona watumishi wa umma hamnazo, wakati ndiyo watendaji wakuu, wakati ndiyo wataalamu wenyewe..

Na mara nyingi changamoto zote wanazokutana watumishi wa umma zinasababishwa ma wao viongozi wa kisiasa..
Well said chief

Na ndio hawa hawa wanaifanya siasa ionekane haina maana kabisa,ndio utasikia kauli kama hii nchi imezidi siasa sana,,,lakini ukweli siasa ndio inatawala maisha yetu ya kila siku

Siasa is about making decision kuna jambo gani linaweza fanywa bila kutoa maamuzi

Sasa kuna haja kubwa sana ya kuwaheshimu watendaji wa ngazi zote
 
Uongozi una misingi yake...

Hawa viongozi wa kisiasa wana tabia ya kuwaona watumishi wa umma hamnazo, wakati ndiyo watendaji wakuu, wakati ndiyo wataalamu wenyewe..

Na mara nyingi changamoto zote wanazokutana watumishi wa umma zinasababishwa ma wao viongozi wa kisiasa..
Shida ya Tanzania siasa ipo juu ya utalaamu ndiyo tatizo linaanzia hapo
 
Huwezi kudharau taaluma ukathamini siasa kama una akili timamu halafu unataka maendeleo
Kweli kabisa taaluma ndiyo inayoleta maendeleo na utaalamu wa kuyandea mambo upo huko

Siasa imepewa thamani kubwa kuliko taaluma ndio maana hata wataalamu wanataka kuingia katika siasa wakapige hela

Lau siasa ingebaki katika misingi yake basi combination ya siasa na taalauma ingeleta mabadiliko chanya sana
 
Siasa inanguvu kuzidi taaluma

Wakati wa corona nadhani mmejionea wenyewe
Ni kweli kabisa Dr
Na ndio maana Mwalimu Nyerere alisema ili tuendelee pamoja na mambo mengine tunahitaji Siasa bora na si bora siasa

Matokeo ya bora siasa kweli tuliyaona
 
Back
Top Bottom