SALOK
JF-Expert Member
- Sep 20, 2011
- 3,364
- 2,001
Wakuu natanguliza shukrani!
Ninatatizo ambalo limeibuka takribani wiki moja ilopita na bado linaendelea, mwanzo niliona kama kitu cha kawaida nikapuuzia ila sasa imekuwa kero sana.
Ni hivi, jicho langu la kushoto linaona mstari uliojikunja kunja hivi, vitu kama vidoti doti vimejipanga. Katikati ya hivyo vidoti kuna kimoja kikubwa cheusi ambapo vingine ni vyeupe. Sasa hicho cheusi ndio kero yenyewe!! Nikiwa kwenye mwanga wa jua ndipo hiyo kero hujitokeza, ama wakati wa usiku na sehemu ya kivuli ni kawaida tu.
Miaka kama mitatu hivi niliwahi kutumia miwani kutokana na maumivu ya kichwa ambapo nilitumia kwa mwaka mmoja, baadae iliharibika na mimi sikwenda kununua nyingine. Kwa sasa sina tena maumivu makali kama ilivokuwa miaka hiyo japo hutokea kwa nadra ktk vipindi fulani fulani.. Hasa nikifanya kazi juani bila ya kuwa na kizuizi kichwani. Kitu kingine huenda ikawa ni sababu ya tatizo hilo nimekuwa mtumiaji wa vifaa vinavyotoa mwanga mkali kama simu nk. Natumaini humu kuna wataalamu wa macho mnaweza kunisaidia.