Jide alijua mapema kuwa ataachika

Hossam

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Posts
3,544
Reaction score
2,169
Ukianza kufuatilia nyimbo zake utagindua huyu mama alijua wazi kwamba hawezi kuishi na captain. Angalia kwa mfano wimbo wake ule 'nani wa kunifuta machozi umeondoka umeenda mbali' kaeleza haya yalotokea na kweli jamaa limeondoka liko mbali sasa! Pili angalia 'wanaume kama mabinti' sasa jamaa naskia anataka mgawo wake! Angalia pia ule wa 'commando binti machozi' alijua hilo!

Nirudi kwa hawa wengine ntataja wachache tu maana napata wali maharage hapa baada ya kuhangaishana na kuku wangu kwenye chanjo!

1. Nature: majina mia kidogo mara kibla mara kiroboto....ona sasa alivyoisha kimtindo. Maana kibla ni kifo na kiroboto dawa yake inajulikana maana ni msumbufu.

2. Prof J: anapenda sana kujitanabaisha kama kiongozi na mzalendo tangu mwanzo kabisa ingawa na yeye hakuficha hisia za mapenzi! Sasa katendwa na hatapenda tena na hivi sasa naskia anataka ubunge! Si mmeona ' ndio mzee'

3. Chid Benz: tangu mwanzo uvaaji wake na manyimbo yake ya kufokafoka kukifanananisha na wanyamwezi kwa kila kitu! Unajua nini kimempata!

4. Belle 9 na Mad ice: tabia yao ya kurembua sauti na unyonge na manyimbo yao ya mapenzi si mmeona? Wote wanahangaika na my wife wao!

5. Mh. Temba: muonekano mavazi na pini zake utaona jamaa anapenda sana misosi na kujiachia! Ndo maana kawahi mno kuvuta jiko ingawa linajuta kuolewa na selebrite dizaini ya Temba, maana jamaa kutwa kucha ni kujimwaga tu!

6. Mr. II alias Sugu: toka mwanzo jamaa lilikuwa linatetea wanyonge tu, kumbuka dizaini ya kama " ipo siku tutaandamana hadi kwa rais tukamweleze hali halisi" hii ilikuwa miaka ya 2000s mwanzoni, sasa jamaa kaibuka kweli bungeni! Kumbuka vizuri wimbo wake wa "hali halisi"

7. Ndomo: yeye pini zake zote ama kusifia madem ama kulalama katendwa! Vaa yake kama mkongo man na kupaka lipstiki kila dem anamuacha, wengine wamemchoka wameamua kudendana na yeye akiona! Jamaa hana dem hadi Leo maana haeleweki!

8. Dully Sykes: tabia yake ya kupenda misifa kaamua kuihamishia kwenye muziki! Jamaa ni kweli anajishebedua sana! Na je uliona wapi lijali ukawa na marafiki warembo kila kona ya mji? Funguka!

9. Blue: tabia ya kupenda makuu na kujiona anazo toka kitambo tu! Wote mmeona anavyojiachia in real life, naskia katika umri huu wake mdogo kishachapa akina onyinye wa bongo kibao tu!

Ongezeeni ila usimpendelee MTU!

Mods, naomba uzi huu msiunganishe na ule wa Jide huu unazaidi ya ujumbe.

Pangu Pakavu.
 
Duh..hapo kwa Belle 9 sijaelewa..maana dogo namkubali kupita maelezo.......vitamin music
 
Duh..hapo kwa Belle 9 sijaelewa..maana dogo namkubali kupita maelezo.......vitamin music

Mimi pia....ila ukisikiliza moja ya kazi yake ambayo pia naikubali ni "masogange" kalalamika sana hapo ukilinganisha na sisi akina pangu pakavu wafatiliaji wa maisha ya maselebrite huku yetu yanatushinda, utagundua jamaa kajiimba kabisaaaa!
 
Wimbo wa masogange ndio ule anaimba Amerudi najuta yote nilofanya kwake.....
 
Hajafikia hatua ya kuitwa Mama kwakua hana mtoto!
 
Mkuu nimekubaliana na wewe.
 
angalia lugha za watu belle na mad ice ( my wife zao)
 
angalia lugha za watu belle na mad ice ( my wife zao)

Ukisoma ujumbe huwa unataka nini, urembaji wa maneno ama ujumbe maridhawa? Nashkuru umeelewa kuwa nilimaanisha my wife zao! Hater wewe
 
Wimbo wa masogange ndio ule anaimba Amerudi najuta yote nilofanya kwake.....

Sort of, samahani kama ntakuudhi kipenzi. Kila penye nyuzi inayomgusaga Jide hakiyamungu lazima utie maguu. Hivi kwa nini? Nimekufuatilia sana sana maana kuna kipindi nilikuwa nakupenda sana but nikaambiwa sjui umewahiwa na ericB52 kama skosei, nikabaki kukupenda kikawaida tu! Samahani sana sana kipenzi kama ntakuudhi ila nilitaka tu kufunga research yangu kwako!
 
Nani alikwambia........., Maana alikupa taarifa isiyo sahihi, Mpenzi wangu ni Vin Diesel

Mie nyuzi zozote huwa natia maguu iwe ya jide au ya nani. Asante kwa kunipenda.

Hakuna uliponikera naamini majibu yangu yatakusaidia kwenye hiyo research yako.
 
Last edited by a moderator:

Dah nimesoma huku natetemeka jamany! Poa wacha nifunge research yangu! Dah kumbe ni Vin hongera zake sana! Mie baada ya kukaa sana humu nikiwa bachelor nategemea sasa kujitangaza hadharani maana nimechoka! Sasa hivi utaona nyuzi mpya, shapm sana wananihadaa tu akina sweetcandle
 
Last edited by a moderator:
Nani alikwambia........., Maana alikupa taarifa isiyo sahihi, Mpenzi wangu ni Vin Diesel

Mie nyuzi zozote huwa natia maguu iwe ya jide au ya nani. Asante kwa kunipenda.

Hakuna uliponikera naamini majibu yangu yatakusaidia kwenye hiyo research yako.

Mbona majanga mpz....huyu ustaadh katokea wapi tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…