Jiepushe na haya mambo kwa gharama yoyote hakuna faida utapata.

Jiepushe na haya mambo kwa gharama yoyote hakuna faida utapata.

Mpira ni starehe yangu kubwa hayo mengine hayana nafasi kwangu.
Pamoja na kuwa ni starehe yangu huwa nayapa nafasi kwani siwezi kutukanana na mtu kisa mpira kufunga safari kupokea timu au kutetea timu pale napoona Kuna makosa ya ama viongozi, kocha au wachezaji.
 
Kuhusu simba na yanga, sio vibaya kushabikia michezo kama hupotezi muda wa kufanya vitu vya muhimu.
Burudani ni hitaji la msingi la binadamu.

Kuhusu CCM na CHADEMA, kama mwananchi ni haki yako(japo mimi nasema ni wajibu) kufuatilia jinsi nchi yako inavyoendeshwa, na ukiona unaweza kubeba jukumu hilo la uongozi katika ngazi yeyote, basi ni haki yako kuwania....

Kufuatilia siasa kunasaidia sana wananchi wajue wanaonewa wapi ili wapaze sauti, na pia watoe michango/maoni mbalimbali.


Hizo hoja zingine sizipingi kwa lolote.
 
Furaha ni jambo muhimu zaidi. Faida ya kuwa na furaha inatosha, si lazima wote tuwe material driven people. SIMBA , YANGA kama inakupa furaha, hiyo ni FAIDA tosha!

NB; unawezaje kumueleza Mbowe kwamba achana na CHADEMA hayo mambo hayana faida wakati hiyo ndiyo kazi yake!
 
Back
Top Bottom