Kuhusu simba na yanga, sio vibaya kushabikia michezo kama hupotezi muda wa kufanya vitu vya muhimu.
Burudani ni hitaji la msingi la binadamu.
Kuhusu CCM na CHADEMA, kama mwananchi ni haki yako(japo mimi nasema ni wajibu) kufuatilia jinsi nchi yako inavyoendeshwa, na ukiona unaweza kubeba jukumu hilo la uongozi katika ngazi yeyote, basi ni haki yako kuwania....
Kufuatilia siasa kunasaidia sana wananchi wajue wanaonewa wapi ili wapaze sauti, na pia watoe michango/maoni mbalimbali.
Hizo hoja zingine sizipingi kwa lolote.