D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,399
- 3,666
Habari wapambanaji wenzangu ntafurahi kujua mko poa na mnaendelea na majukumu ya kimaisha.
Labda wale wa mpaka mwiaho wa mwezi Leo wamepumzika ila wajanja wanaendelea na side hustle.
Jumamosi ya Leo nimeona isipite bila kuandika chochote inaweza kukusaidia au kumsaidia mwingine kikubwa tusinyimane maarifa humu jf
•Nawakumbusha hakuna kukata tamaa mwaka huu umeamua kupambana basi pambana kwelikweli usikate tamaa kwenye maisha ila ukizidiwa badilisha mbinu za mapambano,achana na wajinga wanaosema urudishe mpila kwa kipa hiyo ni Bonge la kosa kwenye maisha.
•Jifunze kujishusha ili upate connection, kuna ile kauli ya maskini jeuri kama vipi iweke pembeni kidogo pale unapotafuta connection ila jishushe kwa mipaka sio mpaka unadharaulika kupitiliza huo utakua uzuzu.
•Jifunze kuhusu fursa kabla hujaikimbilia,tunajua kutake risk ni moja kati ya mambo ya msingi ili uendelee kiuchumi ila basi jifunze kuhusu risk yenyewe kuepuka scams opportunity.
•Afya ndo kila kitu jitahidi angalau ufanye mazoezi basi kila unapopata nafasi hii itakufanya pia uupende mwili wako
•Jitahidi uongeze vyanzo vyako vya mapato
•tumia muda vizuri,punguza kuangalia movie sana,kulala sana,kucheza games sana huo muda unaochezea ipo siku utajutia
•Jijengee utaratibu wa kusoma vitabu na pia miliki diary uwe unaandika mawazo mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi in you are free time.
•umaskini ni mbaya na una gharama na hapa naongelea zaidi umaskini wa kipato(kuna watu wataanza kusema ooh! Kikubwa uhai utajiri upo mbinguni, au hata uwe tajiri lakini utazikwa chini hizi ni akili za kimaskini na kipumbavu piga chini)
•Badilisha taratibu aina ya marafiki ulionao wale wasiokujenga piga chini.
•Connection yako na watu ndio msingi mkuu wa maisha na kumaintain life
Tafuta connection za kukujenga na kukuimarisha watu ambao unajua hata ukikaa nao mkajadili mambo ya msingi kimaisha na kiuchumi lazima utoke na madini ya kutosha hao ndo watu wa kuwa na connection nao,
Kwa humu jf nazungumzia watu kama
Asha D Abinallah
Pascal Mayalla
CHASHA FARMING
JZHOELO
Mkaruka
manengelo
GLOBAL CITIZEN
kinundu (aweke tu mapuuza pembeni ana akili sana ila hapendi kuzitumia akijiongeza atafika mbali)
The Monk
Mwl.RCT
RRONDO (masikhara mengi )
Watu hawa Na wengineo siwezi kuwataja wote nikamaliza ila ni wenye Mawazo chanya na kiukweli huwa naheshimu sana michango yao na point wanazoziandika humu ndani
I STAND TO BE CORRECTED