Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Joeli

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2011
Posts
4,941
Reaction score
3,412
Simu yangu ya htc ilipasuka kioo, nikatafuta weee, mwisho kuna mtu humu jukwaani akanitajia fundi yupo posta anaitwa sele. nikaenda kufika kaniambua kioo kipo ila bei laki, haipungui wala nini, nikaona pagumu.

Mwezi uliopita nikaamua nijaribu ebay nikakuta vioo kibao nikachagua model yangu, nikalipia kwa paypal, kama elfu 36 tu na free shipping.

Baada ya wiki 3 nimekipata kioo.

Kwa wale wanaohofia kuibiwa au kutapeliwa, mie nimepata bidhaa niliyonunua, nanyi msisite kununua.





Mkuu angalia hizi Shipment price toka USA to other countries Bongo tupo Zone M Worldwide Shipping.



Cc: UncleUber

Wakuu habar,nahitaj msaada kwa mfano nimenunua cm online kupitia ebay hiyo cm nitaipokelea wap?? Au nakua najaza kabisa sehem ambayo nitapokelea?? Mfano kama ni sanduku la posta au bandalini??

JIBU: UncleUber replied; mzigo wako utaupokelea posta au mahala popote ambapo utakuwa umeomba mzigo wako upelekwe; mfano unaweza(kama umelipia gharama za kuuleta kwa njia husika) kuja DHL au USPS n.k utaukuta kwenye ofisi husika, mara nyingi uwa wanakupigia simu kifurushi chako kikifika (hata posta wanapiga simu)
 

mkuu umekipokelea wapi? yani hamu yangu kubwa ni kujua process ya shiping ipoje
 
mkuu umekipokelea wapi? yani hamu yangu kubwa ni kujua process ya shiping ipoje

kimekuja na posta, nilitumia slp ya mwanza, so nimekikuta mwanza home nilipofika.

pale jambo la muhimu ni kuangalia wauzaji, wapo ambao wanajulikana, pia angalia shipping bure au unalipia? maana kama shipping ni bure ujue itachukua wiki 3 mpaka 4, kama ni kulipia inachukua less than 7days inategemea wapi unaponunulia.

chief-mkwawa ningeweka picha ya box uone walivyoandika ila kuna jina langu halisi, ntakutumia kwa whatsapp.

cc DecisionMaker
 
Last edited by a moderator:

naomba unielekeze....ulijiungajeungaje na hiyo pay pal.........
 
ebay wanasisitiza utumie paypal kulipa na kataa kama muuzaji ataomba details zako za akaunti ya benki etc.

na nilichopenda ni, wanakwambia kama hujapata ulichonunua siku kumi baada ya muda wa kufikishwa basi waambie ebay na muuzaji ili waweze kujua kimepotelea wapi pia wanaweza kurefund
 
naomba unielekeze....ulijiungajeungaje na hiyo pay pal.........

1. nenda ebay.com kisha register chagua customer au kama wewe ni muuzaji chagua akaunti ya merchant.

2. kujiunga inabidi kadi yako ya benki (visa/mastercard) iwe imesajiliwa kwanza kununua mtandaoni, kisha nenda paypal.com weka details zako na za kadi yako kisha watakutumia verification code (yangu nilichukua crdb) hapo kadi yako itakuwa verified tayari na paypal.

3. nenda sehemu yoyote. wanayokubali paypal nunua chochote, ingiza. detail za paypal, watakata gharama za icho kitu basi umemaliza

very easy
 

Mm eBay nachukuaga sana mizigo
Na bidhaa nyingi nauza humu jf

mkuu chief-mkwawa mm natumia box la chuo hivo silipiagi kitu chochote zaidi ya ile shiping fee iliyoandikwa na muuzaji

Kama alivyo sema chief-mkwawa inabidi kuangalia repitation ya seller

Maana mm kama mnakumbuka nilianzisha thread ya "hivi eBay ni genuine market place" sababu niliona iPhone 5 $14.99 na Mac book mpya $24.99
seller alikuwa wa china na akuwa na positive feedback hata moja
Baada ya dakika na baada ya mm kufanya payment nikaambiwa kwa email, item removed

Namshukuru Mungu nili open case nakikawa refunded lkn hadi leo hii refund sijawahi kuiona kwenye Bank statement naliamua chuna tu

HOPE YOU WILL LEARN FROM WHAT HAPPENED TO ME
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, ni vizuri ungetupa darasa kidogo process nzima maana watu wengi ni wageni na masuala haya ya e-commerce
 

Mkuu maelezo kidogo hapo unapo sema unatumia box la chuo, je kuna mtu hua anakuchukulia au inakuaje, na je ikitokea mzigo wako ukachukuliwa na mtu ambae sio wewe??
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweki mimi hyonktubnaitamani sana mkuu ila ilifika ktk mambo ya paypal nfo nashindwa alafu ktk kuqeka details za kadi pia napo huwa pananizingua sana. Vile vile kuna detals ambazo mtu unataliwa ujaze pale kama za posta. Nikitumia box namba ya home si inafika tu au?
 
me baada ya kupata maelezo kdogo ya hii ebay apa jf nikaamua kuingia kwenye web yao na nkakuta vtu bei cheap sana hasa.malaptops sasa knachonchanganya n kuwa kla nkiclick buy wanaweka selection za nch na Tanzania haimo sasa apo inakaaje? en vp kuhusu paypal coz me nataka nkafungue a/c CRDB na naweza kutumia a/c yang ya TSHS kununua vtu online yaan i mean wafanye exchange wenyewe online?
 

mie natumia akaunti ya shilingi, na laptop zipo ambazo wana ship tanzania
 
mie natumia akaunti ya shilingi, na laptop zipo ambazo wana ship tanzania

Taalifa ambazo zinajazwa PayPal, eBay na Bank lazim ziwe sawa?? mfano Anuani ya posta iliyo jazwa bank ni lazima ifanane na itakayo jazwa ,eBay na PayPal??
pia je wanapokea mabadiliko ya anuani pale mtu atakapo kua kabadili location??
 
Taalifa ambazo zinajazwa PayPal, eBay na Bank lazim ziwe sawa?? mfano Anuani ya posta iliyo jazwa bank ni lazima ifanane na itakayo jazwa ,eBay na PayPal??
pia je wanapokea mabadiliko ya anuani pale mtu atakapo kua kabadili location??

ukiwa unanunua watakuuliza shipping adress iwe sawa na paypal au utabadili, ila details za paypl lazima ziwe sawa na card
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…