Mkuu, ni vizuri ungetupa darasa kidogo process nzima maana watu wengi ni wageni na masuala haya ya e-commerce
mkuu ingekuwa poa mka toa somo vizuri kwa sababu watu wengi wana penda wa fahamu..msaada mkuu
wakuu ni bora mfungue uzi mpya ili mtueleze kwa kiref kuhusu ebay na paypal
Wakuu
ebay ni sehemu ambayo
wauzaji(Seller) na
wanunuaji(Buyer) wanakutana
Muuzaji(Seller) anajiunga kwa kufungua Account
ebay na kisha anatangaza kitu anachokiuza akiwa popote pale Duniani
Mnunuzi(Buyer) anajiunga kwa kufungua Account
ebay popote alipo Duniani kisha anachagua bidhaa nayoitaka iliyotangazwa na
Muuzaji(Seller) ana inunua online.
Ili kukamilisha zoezi la malipo na kuuziana bila kuibiana ndio sasa anaingia
Pay pal
Pay Pal ni njia ya malipo ambapo mtu yeyote anajiunga ili mradi awe ni mteja wa Bank inayotoa Card za
Master au Visa Card
Kibongo Bongo CRDB wapo vizuri, baada ya kufungua Acc na kupewa
Master/Visa Card yako unarudi tena CRDB kuomba wai link
Master/Visa Card yako iweze kufanya online Transaction kwa kujaza form maalumu then you're done
Baada ya kadi yako kuwa Linked unajiunga kwa kufungua Acc
Pay Pal kwa maana ya kwamba unawapa details za Account yako na kuwapa ruhusa kutoa pesa kwenye account unapo waomba kufanya hivyo
Jinsi ebay na Pay Pal wanavyofanya kukamilisha mpango mzima
ebay ni kama soko ambalo watu hawaonani, mmoja yupo Hong Kong anauza iphone mwaingine Yupo Manzese Tz anataka kuinunua lakini wanakuta online through
ebay. so huwezi ukamtumia tu mtu hela kwenye acc ya bank maana anaweza kuingia mitini na asiwepo wa kufuatilia
Sasa wanapotaka kulipana
Pay Pal anaingia katikati
kama bima wa malipo kwa kuhakikisha anamjua vyema
Muuzaji(Seller) ambaye ndio
mlipwaji
Mlipaji aka
Mnunuzi(Buyer) aliyeko Manzese hamlipi direct mlipwaji aka
Muuzaji(Seller) aliyeko Hong Kong,
Anachofanya
Mnunuzi(Buyer) anampa ruhusa
Pay Pal atoe pesa kwenye Acc yake ya bank kutumia
Master/Visa kisha amlipe
Muuzaji(Seller)
Kwakuwa
Pay Pal anakuwa amechukua dhamana ya malipo ya mauziano yenu anawajibika kuhakikisha
Muuzaji(Seller) ana bidhaa kweli anayouza na anaaminika atatuma kwa
Mnunuzi(Buyer) kile alicho tangaza,....Fail to do so basi
Pay Pal atawajibika kumrudishia
Mnunuzi(Buyer) pesa yake, na baada ya hapo
Pay Pal kushirikiana na
ebay ndio watao mtafuta na kumbana
Muuzaji(Seller) kwa utapeli alioufanya lakini wewe utakuwa tayari umerudishiwa pesa yako iwapo watajiridhisha kuna uvunjifu wa makubaliano.
CHANGAMOTO
Mara chache sana inaweza kutoke
Muuzaji(Seller) akawa tapeli maana ili uwe Muuzaji ni lazima lazima
ebay na Pay Pal watataka kujirisha lakini changamoto ipo baada ya kurudishiwa pesa zako
Mifumo ya
Pay Pal yetu wanasema hairuhusu kupokea Pesa maana mabank nasikia sijui hayajaingia mikataba gani I dont know, so kibongo bongo acc zetu za pay pal ni kwa kulipia tu na si kupokea pesa(wataalamu watatusaidia katika hili)
Jambo lingine ni wizi wa mizigo Posta, binafsi ni muhanga wa hili.
Mwaka juzi niliagiza BlackBerry yangu lakini ilipotelea Posta na sijaipata hadi leo, nilianza kumsumbua Buyer lakini alinithibitishi mzigo umetumwa na hadi tarehe ulipopekelewa Bongo, nilipo wabana Posta wakaanza kunizungusha tu.
Na hii ndio maana Buyer wengi hawatumi(ship) mizigo Africa maana Posta za kiafrica ni majanga kwa wizi na hasa ukituma vitu vidogodogo vya thamani ya kuonekana kama Simu kamera nk, mara nyingi wana iba
Kuna baadhi ya items ukiagiza utakutana na mkono wa TRA, hawa jamaa ni wasumbufu balaa ukiingia kwenye kumi nanane zao, watakutwanga makodi hadi uchanganyike au la sivyo ukate
"kitu kidogo"
Hakikisha unaangalia Feed back na Reputation ya
Muuzaji(Seller)
Hakikisha unasoma kwa makini na kuelewa discription ya item, ikiwezekana muulize Buyer kama hujaelewa.
Epuka kutumia njia zingine zaidi ya Pay Pal kama means ya malipo.Unaweza ku bid item alafu ukashangaa unapoke email ianakuambia ipo items kama hiyo kwa bei ndogo......usi jaribu
Shipping nayo ni topic ndefu kidogo natumai wapo wadau wataifafanua vizuri