Jifunze jinsi ya kupanga bei kulingana na aina ya bidhaa unayouza

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
PRICE ELASTICITY OF DEMAND

Hapa tunaongelea jinsi gani ambavyo bei ya bidhaa inaweza athiri uhitaji wa hio bidhaa (demand).

Inaeleza jinsi tabia ya mteja inavyobadilka kulingana na bei ya bidhaa.

Kwenye sheria ya demand inasema kwamba bei inavyoongezeka basi ni lazima demand ya kitu ipungue.

Ila tukasema kuna sababu ambazo zinaweza fanya isiwe hivyo kama mazingira, kipato nk

Sasa kuna aina za price elasticity ili ikusaidie kujua bidhaa gani ipo katika kundi gani.

1. ELASTIC DEMAND

Hapa inaelezea kwamba kitendo cha bei kupunguzwa kidogo basi itasababisha ongezeko kubwa la demand ya hio bidhaa.

Na ongezeko la bei kidogo basi demand itapungua sana.

Kama mfanya biashara bidhaa yako ipo katika hili kundi basi ni vyema kushusha bei ili kuongeza faida.

Bidhaa nyingi za hapa ni zile ambazo kuna bidhaa nyingi zinazoendana na bidhaa unayouza (substitute goods)

Mfano:

Bei ya vifurushi vya internet, ikishushwa kidogo basi watumiaji wataongezeka maradufu

Mfano 2:

Bei ya BOLT ilivyoshushwa kidogo imesababisha ongezeko kubwa la wateja wa BOLT

2. UNITARY ELASTICITY

Hapa tunaongelea kwamba bei ikiongezeka kwa asilimia 10 basi na wateja watapungua kwa asilimia 10.

Bei ikipungua kwa 20% basi wateja wataongezeka kwa 20%

Hamna kitu kama hichi duniani kwasababu tabia ya mwanadamu haipo constant hivyo.

3. INELASTIC

Hapa tunaongelea kwamba bei inavyoongezeka kwa kiasi kikubwa basi wateja watakaopungua kununua hii bidhaa ni wachache.

Pia bei ikipungua kwa kiasi kikubwa basi wateja watakaoongezeka ni wachache.

Kama mfanya biashara bidhaa yako ipo katika hili kundi basi ni vyema kuongeza bei ili kuongeza faida.

Kwamfano:

Prestige goods, watumiaji huangalia ufahari na sio bei.

Kama wanunuaji wa diamond ring hata zikipanda bei bado wataendelea kununua wengi.

Hii pia hutokana na bidhaa kukosa kitu ambacho kinaendana nacho kwahiyo ushindani ni mdogo.

4.ZERO ELASTIC (PERFECTLY INELASTIC)

Hapa ni kwamba hata bei ikiongezeka basi watumiaji ni walewale kama ambavyo bei ikipungua.

Hii pia haipo duniani japo kwa kiasi kidogo necessity gods zinaingia hapa.

Mfano wenye asilimia kadhaa kwenye hii aina ya demand ni

vilevi kama sigara, pombe, madawa ya kulevya nk

5. PERFECTLY ELASTIC

Hapa ni kwamba ongezeko kidogo la bei litafanya watu kutokununua hi bidhaa kabisa, na punguzo kidogo la bei litafanya watu kununua kupitiliza kwa hio bidhaa.

Hii concept pia ni ya kufikirika hamna kitu kama hichi duniani.

Tuelewane Elastic na Inelastic ndio ambazo zinatumika hizo nyengine ni za kufikirika.

Karibuni kuchangia mada.

#priceelasticityofdemand #inelastic #elastic #uchumi #economics

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…