SURA YA KWANZA: HISTORIA, UMUHIMU NA AINA ZA SOYA
Historia ya zao la Soya nchini Tanzania Soya (Glycine Glycine max max) ni zao la jamii ya mikunde. Zao hilo asili yake ni nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800 iliyopita. Zao la soya liliingizwa nchini Tanzania mwaka wa 1907 katika maeneo ya Amani mkoani Tanga. Kati ya miaka ya 1930 na 1960, kilimo cha soya kilipanuka na kuenea hadi maeneo ya Nachingwea mkoa wa Mtwara, Kilosa mkoa wa Morogoro na Peramiho mkoa wa Ruvuma. Kuenea kwa zao hilo katika maeneo hayo kulitokana na msukumo wa mashirika ya Overseas Food Co-operation – (OFC), State Trading Cooperation (STC), General Agricultural Production for Export – (GAPEX) na National Milling Corporation – (NMC).
Mashirika hayo yalisafirisha soya kwenda katika nchi za Japan na Singapore. Kwa kuwa uzalishaji wa zao hilo katika mikoa hiyo ulilenga soko la nje, wananchi hawakufundishwa matumizi yake na kwa sababu hiyo baada ya mashirika hayo kuacha biashara ya zao hilo kilimo cha soya kilifi fi a hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 ambapo uzalishaji ulianza tena baada ya jamii kuhamasika katika matumizi ya soya hasa katika kutengeneza vyakula vya watoto.
Umuhimu wa zao la Soya
Soya ni zao lenye virutubisho vingi vya aina ya protini ikilinganishwa na virutubisho vya aina hiyo katika mazao mengine ya mimea na hata katika baadhi ya vyakula vinavyotokana na wanyama kama nyama na mayai na maziwa.
Sifa hizo za soya zinafanya zao hilo, kuwa na umuhimu wa kipekee katika kutengeneza vyakula vya binadamu na mifugo na matumizi katika viwanda vya madawa na matumizi mengineyo.
Mafuta yatokanayo na soya hayana lehemu (cholesterol) na hivyo kuwa na sifa ya kuboresha afya ya walaji.
Zifuatazo ni faida za kutumia soya:-
i. Soya ina virutubisho vingi na vilivyokamilika vya aina ya protini ambayo ni muhimu katika kuboresha lishe na afya kwa binadamu na mifugo;
ii. Soya ni chanzo rahisi na chenye gharama nafuu cha protini ambacho hata mtu wa kipato cha chini anaweza kumudu kwa kuwa zao hilo linaweza kulimwa maeneo mengi hapa nchini;
iii. Kwa kuwa soya ina kiasi kikubwa cha protini ikilinganishwa na nyama na mayai na maziwa, inasaidia kupunguza kasi ya mashambulizi ya vijidudu vya maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya kansa, moyo, na kuwaongezea nguvu wagonjwa hasa wa UKIMWI;
iv. Soya ni zao muhimu kwa watu wa kipato cha chini katika kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto kwa kuwa hawawezi kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama na mayai;
v. Kutokana na uwingi wa protini, matumizi ya soya kwa watoto yanasaidia viungo kukua kwa haraka;
vi. Soya hurutubisha udongo kwa kutumia njia ya nitrogen fi xation. Kwa hiyo ni zao linalofaa kutumika katika kilimo cha mzunguko (crop rotation) na katika kurutubisha ardhi ;
vii. Soya huongeza kipato na ni zao linaloweza kuchangia katika kuondoa umaskini kwa mkulima kutokana na gharama ndogo za uzalishaji. Aidha, ni zao linaloweza kuondoa umaskini kwa watengenezaji wa vyakula vya binadamu na mifugo, wafanyabiashara na wafugaji na kutoa ajira kwa rika zote yaani vijana na wazee, vijijini na mijini; na
viii. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa mafuta ya soya yanaweza kutumika kwa kuendeshea mitambo yaani bio-fuel na bio-diesel. Aina za Soya Kuna aina mbalimbali za soya; aina zilizozoeleka Tanzania ni pamoja na Bossier, Uyole soya 1, Ezumu Tumu, Delma Hermon, Duiker na Kaleya.
Kila aina inahitaji mazingira na hali ya hewa ina- koweza kustawi, kukomaa kwa muda maalum na kutoa mavuno mazuri. Hata hivyo Bossier ni aina ambayo hustawi katika mae- neo mengi nchini.
Kwa wastani, aina mbalimbali za soya huchukua wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na aina, mahali ilikopandwa na utunzaji katika shamba...