Atkins Mendel
JF-Expert Member
- Feb 12, 2017
- 616
- 755
Mkuu naomba kuulizia kitu kama hutojali, mimi pia nipo Tanga huku Korogwe, nimekuwa nikijishughulisha na kilimo cha maharage haya ya njano, ila kuanzia mwezi wa 10 ninataka kujaribu kilimo cha nyanya. Je kwa uzoefu wako mbegu hii ya Assila f1 kwa upande huu inafanya vizuri? Ukizingatia muda tunaolekea ni msimu wa joto ila nategemea kulima kwa kumwagilia, na je kama Assila haifanyi vizuri huku Tanga ni mbegu gani nyingine ya kisasa (hybrid ) inayokubali huku hasa Korogwe kama unaufahamu nako? Nimefwatilia huku wengi wanatumia mbegu hizi za kawaida kama vile Tanya na Tengeru ambazo wadau wanasema mavuno yake ni kidogo. Msaada wenu wakuu kwa mtu anayefahamu mazingira haya ya Korogwe joto lake linarange kwenye 27 centigrade mpaka 30 centigrade kama Dar es Salaam vile ila udongo wake ni mweusi na una kichanga kwa mbali sana. Je mbegu ya Assila f1 inaweza kuhimili hiyo hali ya hewa?Jamani Bei ya Nyanya ikoje huko Masokoni? kwa maana Huku niliko (Tanga) Bei ni Maumivu, Creti linaenda mpaka elfu kumi (10) Na nikicheki shambani zianiva kwa fujo. Kichwa kimepata Moto.