Jifunze kingereza fasah hapa kwa miezi 2 tuu

Jifunze kingereza fasah hapa kwa miezi 2 tuu

Psiteshio72

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2016
Posts
634
Reaction score
442
Jifunze nami kingereza kwa kiswahili kwa bei cheee, kwa mwezi. Masomo ni online na ni kwa miezi miwili 2,Tunasoma kwa video, pich, audio no kupitia WhatsApp peke,Nipigie sasa na utokwe na aibu ya kutojua kingereza fasah ingali wew ni msomi, many a bias hara ama mtendaji wa serikali,Piga 0753093869,baada ya kuhitimu tutakupatia ajira ukitaka, katika mataw yetu yotee... Mfano wa masomo yetu:

Somo la 1

(SECTION A; TENSES IN THE ACTIVE VOICE )

(A)Simple Tenses ,:

1. Simple Past Tense ( ‘li’)
- Wakati huu huongelea jambo lililofanyika na kukamilika mara moja wakati uliopita.
Mifano ; tulikuja ,walitembea, alicheza.
- Wakati huu huashiriwa na silabi ‘li’ ambayo hufanya tutambue kuwa tunaongelea jambo lililofanyika mara moja na likamalizika kufanyika katika wakati uliopita. Hii silabi ‘li’ ni lazima iunganishwe na kitendo moja kwa moja kabla ya kitendo. Mfano ; ‘Tuliimba’, tofauti na ‘Tulikuwa tunaimba’ ambapo ‘li’ imefuatiwa na kifungu ‘kuwa’ na sio kitendo. Katika maneno ‘tulikuwa tunaimba’, kitendo ‘imba’ kimetanguliwa na ‘na’ na sio ‘li’ kwa hivyo maneno hayo hayapo katika wakati huu wa Simple Past Tense, ‘li’.

Kanuni za kutumia Simple Past Tense ‘li’

a) Sentensi za taarifa/kutoa taarifa
Katika wakati huu, huwa tunapoelezea jambo tunatanguliza mtendaji wa jambo, (I/We/You/They/He/She/It) kisha tunafuatisha kitendo moja kwa moja kikiwa katika umbo la wakati uliopita.
Mfano ; - kitenda ‘enda’ ni ‘go’. Umbo lake la wakati uliopita, yaani ‘-lienda’ ni ‘went’. Tutatanguliza mtendaji wa jambo kisha tufuatishe neno ‘went’.

Sentensi za mifano;
- Juma alienda. ………. Juma went.
- Tulienda. ……… We went.
- Basi liliondoka. ……. The bus left.
- Nilicheza. ……. I played.
- Uliimba. ….. You sang.
- Walikimbia. ….. They ran.
- Maria alipika. ……. Maria cooked.
NB : Hatuweki kitu chochote katikati mwa mtendaji na kitendo.

b) Kuuliza maswali katika Simple Past Tense

- Maswali katika wakati huu huanzia na neon ‘did’. ‘Did’ ikitumika ni lazima kitendo kiwe katika umbo la kawaida kwa sababu ‘did’ ina ‘li’ ndani yake hivyo ‘li’ nyingine haihitajiki. Ina maana hiyo ‘did’ tayari imeshawakilisha wakati uliopita.
- ‘Did’ hufuatwa na nafasi inayouliziwa swali.
Mifano ya tafsiri :
- ‘Did Juma _______ ?’ …….. ‘Je, Juma ali______?’
- ‘Did they _______ ?’ ………. ‘Je, wao wali______ ?’

Sentesi za mifano :

1. Did Juma go?
Je, Juma ali enda ?

Jibu ; ( Hapana, hakuenda)…..( Kukanusha)
No, he didn’t go.
Au ; ( Ndio, alienda)…. Kukubali
Yes, he went.

2. Did she cook?
Je, alipika?

Jibu ; ( Hapana, hakupika)…..Kukanusha
No, she didn’t cook.
Au ; Ndio, alipika….. (Kukubali)
Yes, she cooked.

** katika kitabu kuna michoro ambayo inaonyesha tafsiri ya moja kwa moja ya kila kipengele cha sentensi kutoka kiswahili hadi kingereza ila hapa hatujaionyesha.

NB ; Tukiongeza neno ‘did’ katikati mwa jibu la kukubali, huwa ni kuweka msisitizo kama vile ambavyo kwa Kiswahili huwa tunaandisha sauti ili kuweka msisistizo ila sasa kwa Kingereza sauti haipandishwi ila msisitizo upo pale pale.

Mifano ; 1. Did Juma go ? …… Je, Juma alienda?
- Yes, he did go. ….. Ndio, alienda! (KWA MSISITIZO)

2. Did they cook? …….. Je, walipika?
- Yes, they did cook. …… Ndio, walipika! (KWA MSISITIZO)

NB ; Tunapokanusha sentensi kwa kutumia ‘did not’/ ‘didn’t’ , huwa hatutumii kitendo kikiwa katika umbo la wakati uliopita maana ile ‘did’ inakuwa imeshawakilisha wakati uliopita (‘li’ ambayo kinume chake ni ‘haku’) kwa hivyo hatuhitaji wakati uliopita kwa mara ya pili. Tukitumia umbo la wakati uliopita pia kwa kuuliza swali lililoanzia na ‘did’ pia tunakuwa tumeweka ‘li’ mbili katika sentensi, jambo ambalo sio sahihi.

Mifano ; 1. She didn’t went yesterday. ( Badala ya ‘She didn’t go yesterday.’)
Haku lienda jana. ( Badala ya ‘Hakuenda jana.’)

Au; 2. Did she went yesterday?
( Badala ya ‘Did she go yesterday?’)

- Je, yeye ali lienda jana?
( Badala ya ‘Je, yeye alienda jana?)
 
Kwa full course nipigie, pia ni rahis kujifunza WhatsApp utajua ni namna gani ya kutamka maneno
 
Neno "we're" hutamkwa "waa"
Mfano
They were eating.
Zeyi waa iting
Wewe unajua, nimekutana na wengi hilo neno hutamka "weya"
Je vp wale haya maneno wanamalizia na o
Table - tebo?
Little - lito?
Coral - Koro?
Kettle - keto?
 
Utamkwaji wa maneno haya
Were -waa
Where-weya
Wear-wea
 
Pia neno "university" hutamkwa yunivesti na sio yunivasitiyi..
Pia neno hilo hutumia article /kiashiria "a"
Sababu 3
Kwanza ukilitamka huanzia na sauti ya konsonanti "yu"na sio "u"
Pil lina wingi..
Tatu sio jina LA mtu au la mahali
 
Pia neno "university" hutamkwa yunivesti na sio yunivasitiyi..
Pia neno hilo hutumia article /kiashiria "a"
Sababu 3
Kwanza ukilitamka huanzia na sauti ya konsonanti "yu"na sio "u"
Pil lina wingi..
Tatu sio jina LA mtu au la mahali
Hata wewe naona unahitaji upingwe brush ya English course, huwezi ukaweka phonetics za maneno ya kingereza kwa kiswahili ukiamini mwanafunzi atatamka neno hilo kwa ufasaha.
 
Hata wewe naona unahitaji upingwe brush ya English course, huwezi ukaweka phonetics za maneno ya kingereza kwa kiswahili ukiamini mwanafunzi atatamka neno hilo kwa ufasaha.
Mimi ninachuo kinaitwa "jifunze kingereza kwa kiswahili" hi kurahisisha kwa wale wanafunzi wasioelewa,
Has a watu wazima nikaon ni lazima nitumie kiswahil kma lugha mama. Labda mimi ndo nikufundishe weww, mimi ni mkufunz mpka uganda, egypt nk
 
Hata wewe naona unahitaji upingwe brush ya English course, huwezi ukaweka phonetics za maneno ya kingereza kwa kiswahili ukiamini mwanafunzi atatamka neno hilo kwa ufasaha.
Ni lazima kabisa.
Mfano naomba unitamkie hili neno na maana yake
Have.
 
Mimi ninachuo kinaitwa "jifunze kingereza kwa kiswahili" hi kurahisisha kwa wale wanafunzi wasioelewa,
Has a watu wazima nikaon ni lazima nitumie kiswahil kma lugha mama. Labda mimi ndo nikufundishe weww, mimi ni mkufunz mpka uganda, egypt nk
Huwezi kupata pronunciation sahihi kwa unavyofanya. Ukienda katika nchi za Asia na kingereza cha pronunciation za kiswahili wachache watakuwa wanakuelewa, kwa nchi zinasongea kingereza wengi watakuelewa.
 
Huwezi kupata pronunciation sahihi kwa unavyofanya. Ukienda katika nchi za Asia na kingereza cha pronunciation za kiswahili wachache watakuwa wanakuelewa, kwa nchi zinasongea kingereza wengi watakuelewa.
Mkuumimi sio mbabaishi embu soma kwa makini hapa
Nimefundsha zaid ya nchi 7 njee
Kwanza lugha hi kila nchi in a lafudhi yake, pili kumbuka kingereza safi hutokea Uingereza, marekani cha kihuni,
Ndo maana tunasema jifunze kingereza fasaha... Hatujifunzii kingereza cha kenya, wala marekani... Mimi ninatamka maneno kiusahihi niwe hata Dubai na wazungu nawakosoa mfano
Neno Tepic-utamkwaji wa neno hili linategemea nchi na nchi katika lugha ila kwa ufasah huwa lina maana 1 kiutamkwaji, tofauti za nchi kutaamka ni lugha waitumiayo
Tepic, "c" hutamkwa kma "k" pia "ch" ni nchi ipi na ni kwa lugha gani uitumiayo????
Kwa tz ni lazima mimi nitumie kiswahili kwa maana kingereza nchi hi ni tatizo kubwa, na hizo ni mbinu za Mwalimu.
Nikifundisha labda Oman-nitatumia kingereza tuuu.
 
Mkuu nilikua naomba garama zako hata kwa pm
Ni muhitaji mno wa kujua lugha ya kiingereza. Pia naomba maelekezo ni namna gani ya mnafundusha na muda gani na malipo ni ya namna gani. Japo ki financial sipo vizuri lakini nina nia mno. Kila la heri
 
Back
Top Bottom