Jifunze kuhusu Mashahidi wa Uganda

Jifunze kuhusu Mashahidi wa Uganda

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Wafiadini wa Uganda

Nchi ya Uganda iliwahi kupatwa na dhuluma dhidi ya dini, hasa Ukristo, hususan madhehebu ya Anglikana na Kanisa Katoliki. Waliouawa katika mazingira ya namna hiyo, wanaitwa wafiadini, kwa hiyo wafiadini wa Uganda.

Wafiadini wa karne ya 19. Watakatifu hao wanaonyeshwa katika filamu "Millions".

Wafiadini Wakatoliki

Karolo Lwanga katikati ya wenzake 21 wa Kanisa Katoliki katika mchoro wa Albert Wider wa mwaka 1962.

Kati yao wanajulikana na kuheshimiwa duniani kote kwa namna ya pekee Wakatoliki 22 waliokuwa wahudumu wa ikulu ya kabaka wa Buganda Mwanga II (1884 - 1903) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na kardinali Charles Lavigerie.

Ndio wafiadini wa kwanza wa kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu. Majina yao ni haya:

Yosefu Mukasa Balikuddembe († Nakivubo, 15 Novemba 1885), wa ukoo Kayozi, wa kwanza kuuawa akiwa na miaka 25.

Andrea Kaggwa († Munyonyo, 26 Mei 1886), wa kabila la Banyoro, ndugu wa mfalme.

Ponsyano Ngondwe († Ttakajjunge, 26 Mei 1886), wa ukoo Nnyonyi Nnyange.

Dionisi Ssebuggwawo († Munyonyo, 26 Mei 1886), wa ukoo Musu.

Atanasi Bazzekuketta († Nakivubo, 27 Mei 1886), wa ukoo Nkima.

Gonzaga Gonza († Lubowa, 27 Mei 1886), wa ukoo Mpologoma, kabila la Basoga.

Matias Mulumba Kalemba († Kampala, 27 Mei 1886), wa kabila la Banyoro, ukoo Lugave.

Noe Mawaggali († Mityana, 31 Mei 1886), wa ukoo Ngabi.

Karolo Lwanga († Namugongo, 3 Juni 1886), wa ukoo Ngabi. Pamoja naye waliuawa hawa wafuatao:

Luka Banabakintu (miaka 35), wa ukoo Mmamba;

Yakobo Buzabaliawo (miaka 25), wa ukoo Ngeye;

Gyavira Musoke (miaka 17), wa ukoo Mmamba;

Ambrosi Kibuka (miaka 18), wa ukoo Lugave;

Anatoli Kiriggwajjo (miaka 20), wa kabila la Banyoro;

Mukasa Kiriwawanvu (miaka 20), wa ukoo Ndiga;

Achile Kiwanuka (miaka 17), wa ukoo Lugave;

Kizito, kijana kuliko wote, kwa kuwa alizaliwa mwaka 1872, wa ukoo Mmamba;

Adolfo Mukasa Ludigo (miaka 24), wa kabila la Banyoro;

Mugagga Lubowa (miaka 16), wa ukoo Ngo;

Bruno Sserunkuma (miaka 30), wa ukoo Ndiga;

Mbaga Tuzinde (miaka 17), wa ukoo Mmamba.

Yohane Maria Muzei, mzaliwa wa eneo la Kagera (Tanzania ya leo), wa mwisho kuuawa († Mengo, 27 Januari 1887) akiwa na umri wa 30.

Katika ibada ya kuwatangaza hao (1964), Papa Paulo VI alitaja pia kwa jumla wafiadini wengine wa dhuluma hiyo waliokuwa wa madhehebu ya Anglikana.[1] .

Wafiadini wa Anglikana

Labda ni wengi zaidi Waanglikana waliouawa katika dhuluma hiyo, kuanzia Yusufu Lagamala, Mark Kakumba na Noah Seruwanga waliokatwakatwa vipandevipande na kuchomwa moto tarehe 31 Januari 1885.

Waliofuata ni askofu James Hannington na wenzake waliouawa tarehe 29 Oktoba 1885 kabla hawajaingia Buganda. Mwaka 1886, kati ya tarehe 25 Mei na 3 Juni, waliuawa: Moses Mukasa (kwa mkuki), Muddwaguma na Elias Mbwa (kwa kuhasiwa), David Muwanga (tarehe na aina ya kifo chake haijulikani), Omuwanga, Kayizzi Kibuka, Mayanja Kitogo aina ya kifo chao haijulikani), Alexander Kadako na Frederiko Kidza (kwa kupigwa), Noah Walikaga , Daniel Nakabandwa, Kiwanuka Gizayo, Mukasa Lwa Kisiga, Lwanga, Mubi, Wasswa, Kwabafu, Kifamunyanja, Muwanga Njigija (wote kwa kuchomwa moto), Robert Munyagabyanjo (kwa kukatwakatwa vipandevipande na kuchomwa moto).

images - 2020-06-03T194121.353.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapumzike kwa amani mahali pema peponi

Jr[emoji769]
 
stephen4440,

Hii ni sehemu ya madhara ya ukoloni kwa waafrika, hawa ni waafrika waliouliwa na viongozi wa Afrika baada ya kuasi amri na taratabu za viongozi wa Africa na kuwafuata wakoloni wa kizungu, vipi sisi waafrika tunawatuka? Hawa walipaswa kutukuzwa na wazungu sio Waafrika.

Kuna waafrika wengi sana waliouliwa na wakoloni kwa kukataa kutii amri zao, hao ndio tulipaswa tywatukuzi kama ambavyo wamarekani weusi wanavyomtukuza "Martin Lutherking Jr.

Jambo la kushangaza ni kuona kwamba waafrika waliouliwa na wazungu kwa kugoma kutii amri za wazungu hatuwakumbuki badala yake tunawakumbuka waafrika walioungana na wazungu kupinga amri za viongozi wa Kiafrika. Huu ni muendelezo wa utumwa wa kifikra.
 
Back
Top Bottom