Jifunze kukaa kimya hakuna matatizo ya kudumu

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Pablo Escobar aliwahi kushauri kwamba, si vyema sana kuwaambia watu matatizo yako. Alipoulizwa kwanini alisema ivi, "Asilimia 80 ya watu unaowaambia matatizo yako, hawajali na wala hawazingatii, asilimia 20 iliyobaki wanashukuru au wanafurahia wewe kuwa na hayo matatizo uliyonayo".

Rafiki yangu wa muda mrefu sana. Mr Francis, aliwahi kuniambia ivi, "Kashindi, kila mbwa ana stori ya kumwambia mbwa mwenzie ila hakuna mbwa hata mmoja ambaye yuko tayari kukaa chini na kusikiliza stori ya mbwa mwenzie"

Huwa kuna mahali tunakosea sana. Ndiyo, siyo kitu kibaya kumishirikisha mtu matatizo uliyonayo, binafsi nina watu ambao huwa nawashirikisha, mimi pia nimekuwa mshirikishwaji mkubwa sana wa matatizo na changamoto za watu wengi sana na nimekuwa nikitoa ushauri mzuri sana na hata msaada ili tu kuhakikisha shida au tatizo alilonalo mtu linaisha ua kupata majibu yaliyo sahihi.

Tatizo ni pale unapoanza kuhubiri shida zako kwa kila mtu. Siyo kila mtu anafaa kujua matatizo yako. Mwingine akijua shida zako ndiyo moyo wake unapata amani. Ndiyo anafurahi na mpaka anatamani shida ziongezeke kwako ili aendelee kukucheka.

Waswahili husema kwamba, "Chongo hushukuru Mungu anapomuona kipofu".

Lakini pia, siku hizi watu hawako katika mitazamo ya kutatua matatizo badala yake wanaangalia wao wanashida za namna gani kisha wanaangalia nani mwenye shida kama walizo nazo wao, kwa kifupi, tatizo lako unatamani na mwingine awe nalo.

Tujitahidi sana kuwashirikisha shida watu ambao ni sahihi. Tusimwambie kila mtu matatizo yetu kwani kufanya hivyo wakati mwingine ni kujidharirisha. Kila mtu ana shida zake kwahiyo inahitaji hekima kubwa sana kusikiliza shida za mtu mwingine.

Kuna mtu ukimwambia hauna hela, siku hiyo hiyo mtaa mzima unajua kwamba fulani kafulia. Na Kuna mwingine hata kama hana anaweza akakukopea sehemu. Inategemeana na hulka au tabia ya mtu mwenyewe.

Kwa hiyo tujitahidi sana kuwashirikisha shida zetu watu ambao watakuwa msaada kwetu, watu ambao ni sahihi bila kujisahau.

Shida zinaumiza ila ukizihubiri kwa kila mtu unaweza ukaumia mara mbili maana utakachokutana nacho siyo kile unachokitegemea. Utatangazwa kijiji kizima, mtaa mzima mpaka kwa watoto.
 
Unatushauri nini sisi ambao kila maendeleo au hatua tunayopiga tunaweka "status"
 
Noted ukweli mtupu.
 
Uko sahihi tatizo lina tabia ya kutokudumu ila watu wengi wanadhani tatizo linapokuja huwa linakuja kudumu, watu wengi wamejikuta wamezalisha matatizo mapya kwa kutojifunza kunyamaza.
 
Dahh..ila matatizo bwana omba tu uaikutane nayo, au ukikutana nayo yawe yale ambayo unaya manage na yako ndaji ya uwezo wako, vinginevyo utajuta..

Kuna shida zinakupata unaona kabisaa kukaa kimya huwezi, yqn unahis kama una burst hiv, unataman kumwambia kila mtu maana ndio angalau una pata releaf.

Anyway, Mungu atuepushe na matatizo
 
Back
Top Bottom