Hakuna Familia Kamili Hatuna wazazi kamili, nawe pia si mkamilifu, Hatuoi mtu mkamilifu wala hatuna watoto wakamilifu.
Tunalalamikiana. Hatuwezi kuishi pamoja bila kukoseana. Mara nyingi tunavunjika moyo. Ndiyo, kwa sababu nyingi tofauti na nyakati tofauti, tunakatishwa tamaa na wenzetu.
Hakuna ndoa yenye afya wala familia yenye afya bila tendo la msamaha. Msamaha ni dawa ya furaha na amani ya familia Msamaha ni muhimu kwa afya ya hisia zetu na kwa maisha yetu ya kiroho. Haijalishi kosa ni lipi au nani aliyekosea. Bila msamaha, familia hugeuka kuwa uwanja wa vita na ngome ya uovu.
Bila msamaha, familia huwa mgonjwa na isiyo na afya. Msamaha ni usafi wa roho, utakaso wa nafsi na ukombozi wa moyo. Hakuna dhambi iliyo kubwa mno isiyosameheka.Yeyote asiyesamehe hana amani moyoni mwake, wala hawezi kuwa na ushirika na Mungu.
Kukataa kusamehe ni uovu na ni sumu inayomuua yule anayeshikilia chuki. Kuhifadhi maumivu ya kutokusamehe moyoni ni kitendo cha kujiharibu. Ni kujila mwenyewe kwa ndani autophagy. Wale wasiosamehe huwa wagonjwa kimwili, kihisia na kiroho. Na watateseka kwa njia mbili.
Kwa sababu hiyo, familia lazima iwe mahali pa uzima na si mahali pa mauti mahali pa msamaha, mahali pa peponi na si motoni; eneo la uponyaji na si la maradhi; shule ya msamaha na si ya lawama.
Msamaha huleta furaha mahali huzuni ilipokuwa; huleta uponyaji mahali ugonjwa ulipowekwa na huzuni.Familia ni mahali pa kusaidiana na si pa kusengenyana au kubeza.
Lazima iwe mahali pakukaribishana, si pa kukataliwa. Aibu kwa wale wanaopanda uovu juu ya wengine. Sisi ni familia, si maadui.Wakati mtu anakumbwa na changamoto, anachohitaji ni masaada sio kusimangwa.