Jifunze kutafuta sababu fiche kwenye kila sababu inayo onekana kama chanzo

Jifunze kutafuta sababu fiche kwenye kila sababu inayo onekana kama chanzo

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Aliyekuacha kwenye mahusiano kuna uwezekano mkubwa sababu siyo hiyo aliyokwambia bali ni ile aliyokuficha sema kapitia hiyo kama njia ya kufanikisha njama yake ya muda mrefu.

Ulisema tatizo huna kazi baada ya kupata ukahamia kwenye tatizo mshahara mdogo ila ukweli mchungu ni kuwa kuna uwezekano mkubwa tatizo wewe na sio hivyo unavyovipa uhusika wa matatizo.

Mara nyingi tunakwamisha na sababu FICHE ndio maana tunakuwa kwenye hali zetu mbaya kwa muda mrefu kwa sababu tunapambana na adui ambaye madhara yake ni madogo sana na kumuacha adui mwenye madhara makubwa ambaye kajificha nyuma ya huyo adui anayeonekana.

Ukiona jambo unapambana nalo muda mrefu bila mafanikio kaa chini fikiria kwa kina kweli nyuma yake hakuna sababu FICHE?

Unaweza fikiria kakuacha kwa sababu huna pesa ila hata ungekuwa na pesa bado tu angekuacha , pana sababu FICHE hapo.

Mwanafunzi anasoma sana na hana starehe tena hata darasani hakosi Vipindi ila matokeo hayabadiliki , pana sababu FICHE hapo

Sio mbaya kuwa mtafiti kwenye kila sababu unayodhani ndio kikwazo siku ukitatuliwa angalia tatizo linaisha ? Ikiwa linaendelea jua pana sababu FICHE.

Mtu analalamika hana mtaji ila akipewa bado tu mambo magumu hapo pana sababu FICHE.

Mbinu moja wapo ya kutafuta sababu kuu iliyojificha ni kuwa na utaratibu wa kufuatilia historia yako/yake je kweli hicho alichokosa leo na kusema ni sababu hajawahi kuwa nacho kabla na bado akakwama?

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako
 
Back
Top Bottom