Jifunze Kwa waliopita utafanikiwa

Jifunze Kwa waliopita utafanikiwa

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
Charlie Chaplin alipofariki akiwa na miaka 88
aliacha kauli 4:

1. Hakuna kinachodumu milele duniani, hata matatizo yetu.

2. Napenda kutembea kwenye mvua kwasababu hakuna atakayeyaona machozi yangu.

3. Siku iliyotumika vibaya zaidi maishani ni ile siku ambayo hatucheki.

4. Madaktari sita bora zaidi duniani ni...
I. Mwanga wa jua
II. Mapumziko
III. Mazoezi
IV. Mlo bora
V. Kujithamini
VI. Marafiki

Fanya hayo yote katika hatua zote za maisha yako ufurahie maisha bora.
Ukiuona mwezi utauona uzuri wa Mungu.

Ukiliona jua utaona uwezo na nguvu za Mungu

Ukijitazama kwenye kioo, utaona uumbaji bora kabisa wa Mungu

Amini Kuwa
Sisi sote ni watalii, Mungu ndiye anayeratibu safari yetu ambapo amekwishapanga kila kitu, vyumba vya kulala na tutakapoishia.

Mwamini Yeye na furahia MAISHA

Maisha ni safari!

Ishi leo vizuri!


1724679999633.jpg
 
Wanaingiaje tena, ukiuawa utayapata wapi hayo unayotuhubiria, Chaplain amekufa na miaka 88 je wewe ukiuawa na Hawa manyang'au utaacha story gani mkuu?
Dah maisha uloishi ndo stori utakayoiacha
 
Back
Top Bottom