Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sanaHeshima kwanza
Wakuu, nina shamba eneo la Makaa Yamu, Kirua Vunjo, wilaya ya Moshi vijijini lenye ukubwa wa ekari kumi na sita 16 (limepimwa na hati miliki)
Shamba lipo kilometer nne kutoka barabara kuu iendayo Dar es salaam na Mombasa.Shamba hili lipo eneo la ukanda wa tambarare Kusini mwa mlima Kilimanjaro.Ukanda wa eneo hili lilipo shamba langu ni mkubwa sana na wamiliki wengi wa mashamba haya hulima mahindi wakati wa msimu wa mvua (masika).
Eneo hili lina rutuba nzuri sana, udongo wake ni tifutifu. Inaonyesha kuwa water table yake haipo mbali sana.
Wakuu wazo langu ni kugeuza uwanda huu kuwa horticultural hub kwa kilimo cha aina ya zao la matunda ya passion lengo likiwa ni kuweza kusindika tunda hili la passion na kupata passion powder kwa ajili ya flavoring kwenye bidhaa mbali mbali za chakula kama ice creams, cakes, fruit yougurt, juices and soft drinks, jams n.k
Pia tunda hili la passion linaweza kutengeneza wine mzuri sana.
Naomba pia anayejua bidhaa tofauti zinazotokana na zao hili na masoko yanayohusu passion fruit.
Wakuu ninaomba ushauri juu ya utaalam wa ulimaji wa zao la passion, hivyo basi nikiweze kuanzisha kilimo hicho nitatoa mfano wa shamba bora na kuwabadilisha wakulima wote wa eneo / uwanda huu waweze kulima hili zao na baadae kulisambaza maeneo ya nchi nzima ambapo zao hili products zake zina soko lenye bei nzuri na kubadilisha maisha ya wananchi hawa.
Haya ni mawazo tu ya mwanzo ambayo sijayafanyia utafiti wa kina nikisubiri changamoto na michango ya wenzangu wapenda kilimo na wenye utaalam na uzoefu zaidi .
Pia yeyote yule humu JF anakaribishwa kutoa ushauri na mchango wake.
---------------------------------
Asante sana
mbona kidogo au?Nimejaribu hii kitu Kwa kuotesha miche minne mwezi April 2016 jana tar 04 Jan nimepata kiasi cha matunda 20View attachment 454731
Sasa miche minne tu. Anawezaje kupata debe. Afu bado yanazaambona kidogo au?
Miche minne matunda 20?sasa miche minne tu. anawezaje kupata debe. afu bado yanazaa
mbona kidogo au?
Miche minne matunda 20?
Mi najua yanazaa sana ndo maana nashangaa
Amejaribu tu... Ila angepanda Miche 100 angepata 5000.mbona kidogo au?
Wakuu nataka nianze kilimo cha matunda ya passion,naomba mwenye kujua utaalamu wake,masoko na etc. anisaidie