Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

Hiyo ni cake au mkate? wingi wa sukari na mayai unaondosha hilo jina na hivyo kuwa keki

Mkuu kwetu sisi mkate wa maji huko sijui mnaitaje tunaweka hadi 5eggs na chapati pia tunaweka...etc etc na bado tunaiita mikate na kuna mikate ya sukari tunayoweka zaidi ya glass...tunatofautiana mkuu kwa mujib wa maeneo tunayoishi na pia vyakula.
Kwahio hakuna tatizo km ww ukiona mayai na sukari unaona uite cake waweza fanya hivyo.. hapa tunashare taste tu na hilo ndo muhimu...
 
MKATE WA MAYAI

Vipimo

Mayai 4
Sukari ¼ Kikombe
Unga wa Ngano Vijiko 5 ½ vya chakula
Hiliki ya kusaga ½ kijiko cha chai
Baking powder ½ Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, iliki na vunja YAI MOJA BAADA YA JENGINE KWENYE KIBAKULI KANDO NDIPOSA UMIMINE KWENYE BAKULI KUBWA LA SUKARI
2. Changanya sukari, iliki na mayai kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.
3. Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto au makaa..kwa watumiao makaa…
4. Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari.
5. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge. Na kupunguza madonge..chunga unga wako kwa tungio…
6. Mimina unga ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.
7. waweza kuweka karatasi kwa ndani ya sufuria umbo la mduara au kama ni baking tray umbo la mraba kwa kuipakia mafuta ili mkate usishike unapotaka utoa baadae.
8. Ingiza sufuria ndani ya jiko (oven) na oka kwa dakika 20 au 30 vile vile makaa ya chini yawe kiasi tu kuliko ya juu ya mfiniko.
9. Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick. Ingiza kijiti katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.
10. Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.


693770414fead5ada8e833232ac4d8ab.jpg
3f66b1319d22ad4951539ca691fc07f8.jpg
 
1)ivi ni kweli mikate INA amira tofauti na amira nyingine
2)in vitu gan vinaongezwa kiwandan inayofanya mikate ya kiwandani kuonekana bora zaid ya ya nyumbani
 
Hamira na sio amira kwa kuanzia

Pili manjonjo ya mtengenezaji ndio hufanya mkate kuwa tofauti, mfano utiaji wa mafuta, mayai n.k

Hayo tu
 
Ina vikorobwezo ving mikate ten ukiipik mwenyew na hivy vikorobwezo inakuwa mitam zaid
 
Mahitaji
1)Tambi 500g
2) maji 3-4cups
3)sukari 1 cup
4)1/4 hiliki iliyotwangwa
5)tui la nazi 1 cup
6)samli 1 tablespoon.
7)Arki ya rose au flavor yoyote unayopendelea

Namna ya kutaarisha

1)changanya maji,sukari,hiliki na tui la nazi kwenye sufuria
2)weka kwenye moto mdogo mdogo hadi vichemke
3)vunja vunja tambi na uweke
4)pika hadi tui la nazi likauke
5)pakaza samli juu yake
6)washa oven 300°-350° then oka mkae wako....hakikisha unawiva vizuri...

7)mkate wa tambi tayari kwa kuliwa...
mkuu samahani hivi huu mkate jiko la mkaa au gesi naweza kutumia vipi hizi flavour zinaptikana wapi mbali na arki rose flavour zingine ni zipi nashkuru
 
Back
Top Bottom