MKATE WA MAYAI
Vipimo
Mayai 4
Sukari ¼ Kikombe
Unga wa Ngano Vijiko 5 ½ vya chakula
Hiliki ya kusaga ½ kijiko cha chai
Baking powder ½ Kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Chukua bakuli la kiasi, weka sukari, iliki na vunja YAI MOJA BAADA YA JENGINE KWENYE KIBAKULI KANDO NDIPOSA UMIMINE KWENYE BAKULI KUBWA LA SUKARI
2. Changanya sukari, iliki na mayai kwa kutumia mashine ya kukorogea keki (cake mixer), mpaka sukari ivurugike yote na kuumuka.
3. Washa jiko lako (oven) 350F lianze kupata moto au makaa..kwa watumiao makaa…
4. Weka baking powder kwenye unga na uanze kuuchanganya kidogo kidogo kwenye mchanganyiko wa mayai na sukari.
5. Hakikisha kila ukiweka unga kidogo unauchanganya vyema usiwe na madonge. Na kupunguza madonge..chunga unga wako kwa tungio…
6. Mimina unga ndani ya sufuria ya kuchomea keki ya kiasi.
7. waweza kuweka karatasi kwa ndani ya sufuria umbo la mduara au kama ni baking tray umbo la mraba kwa kuipakia mafuta ili mkate usishike unapotaka utoa baadae.
8. Ingiza sufuria ndani ya jiko (oven) na oka kwa dakika 20 au 30 vile vile makaa ya chini yawe kiasi tu kuliko ya juu ya mfiniko.
9. Uhakikishe mkate wako kama umeiva kwa kijiti cha kuchomea mshikaki au toothpick. Ingiza kijiti katikati ya mkate kisha kitoe na ukiguse uangalie kama kikavu mkate umeiva kama bado kuna ubichi basi rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague.
10. Wacha mkate upoe kisha utoe ndani ya sufuria na uweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.