Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,120
Kumekuwa na wimbi kubwa la mahubiri, imani potofu chini ya mwamvuli wa ukristo kiasi cha imani hali ya kikristo kuonekana ni uongo, utapeli, uzushi nk. Athari zake zimekuwa mbaya kwa waumini wengi wa kikristo.
Mwanzoni lilikuwa linaonekana kama ni tatizo la wakristo wachanga tu lakini kwa sasa limekuwa ni tatizo la wakristo wa aina zote hususani waliokosa msingi halisi mafundisho ya ukristo.
Kabla ya kuendelea mbele, nataka kuweka sawa hapa, ukristo halisi ni ule unaojengwa katika Yesu kristo yeye pekee na ukitumia neno la Mungu pekee yaani maandiko ya biblia.
Haya nayaandika nikizingatia angalizo muhimu ambalo Yesu mwenyewe alilitoa kuelezea dalili za siku za mwisho. (Mathayo 24:1-51)
Hapa chini ni mbinu rahisi, rafiki na halisi za mtu yoyote kuweza kutumia katika kuyapima mahubiri, kumpima mhubiri na kuzipima imani zozote zinazokuja na mwamvuli ya ukristo.
Kwa kifupi sana Injili ya Yesu kristo ndio Ukristo wenyewe, na Injili ya Yesu maana yake habari njema za UFALME wa Mungu kwa watu wote, tunazozipokea kwa njia ya IMANI kupitia YESU kristo pekee kwa kuhabarishwa kupitia NENO la Mungu na kuziishi kwa UPENDO ili kuwa WATAKATIFU.
Hivyo vipimo rahisi vya Ukristo ni YESU, NENO, IMANI, UFALME, UTAKATIFU na UPENDO Na hivyo ndivyo tunaweza kwa uchache kuvitumia katika kuwapima wahubiri, mahubiri na imani zozote zinazohubiriwa chini ya mwamvuli wa ukristo.
Ufafanuzi wa kina upo hapa chini;
1. YESU KUHUBIRIWA YEYE PEKEE YAKE. (Yohana 14:6)
Hakuna Yesu, hakuna ukristo. Mahubiri yoyote yaliyolenga kumuinua au kumtukuza mtu fulani tofauti na Yesu, dhehebu fulani, imani fulani hayo sio mahubiri ya kumuinua Yesu, huo sio ukristo, bali ni utapeli wa kutumia mwamvuli wa ukristo. Kwa mfano, mahubiri ya kutakiwa kuomba kupitia mtu fulani, nabii au mtu fulani, mfu fulani, mhubiri fulani hayo ni mahubiri potofu katika ukristo.
2. UFALME WA MUNGU KUHUBIRIWA KWANZA NA KUSISITIZWA WAKATI WOTE WA MAHUBIRI. (Mathayo 6:33)
Ufalme wa Mungu ni mfumo wa maisha inaotaka kila kitu katika maisha yetu ya kila siku kifanyike kwa lengo la kumuinua na kumtukuza Mungu kupitia jina la Yesu kristo pekee.
Mahubiri yoyote yanayoeleza namna ya kufanikiwa katika maisha yetu kwa njia ya imani lakini yanakwepa msingi wa Yesu kristo kuinuliwa kwanza katika maisha yetu, hayo ni mahubiri ya kitapeli. Kwa mfano, mahubiri ya kuombewa kupata utajiri tu, kupata watoto, kupata mwenza, kupata kazi, kupona magonjwa nk. lakini hayataki Yesu ainuliwe kwanza (Yesu awe sehemu ya maisha ya kila siku moja kwa moja kwa mhusika) ni mahubiri ya kitapeli.
3. YESU KUHUBIRIWA KIIMANI BILA KUWEKEWA MIPAKA FULANI YA KIDINI. (Yohana 3:16, Ufunuo 3:20)
Yesu alikuja kwa kila mtu, hivyo mtu yoyote anaweza kumwamini Yesu popote alipo, Yesu anaweza kumfikia mtu yoyote yule, popote pale alipo na kumpa msaada. Mahubiri yoyote yanayokuwekea mipaka ya wewe binafsi kumfikia Yesu kristo au kushindwa kupata msaada wa Mungu kupitia Yesu kristo hayo ni mahubiri ya kitapeli.
Kwa mfano, mahubiri yanakutaka utoe sadaka kwanza, utumie vitu fulani fulani (maji, chumvi, mafuta nk), uwe muumini wa dhehebu fulani kwanza, ufanye matendo fulani fulani ya kimapokeo kwanza, uombewe na mtu fulani kipekee ili Mungu akusaidie hayo ni mahubiri ya kitapeli.
4. NENO LA MUNGU PEKEE KUTUMIKA KAMA MSINGI WA MAHUBIRI.(Yohana 1: 1-14, Matendo ya Mitume 17:11, ).
Mhubiri yoyote au mahubiri yoyote ni lazima rejea yake iwe kwenye neno la Mungu tu. Nje ya hapo ni hadithi za kutunga na imani zingine ambazo sio ukristo.
5. UTAKATIFU KUWA MSINGI WA KUPIMA MAHUBIRI NA MAISHA YA MHUBIRI. (Mathayo 7:15, 1Petro 1:15-16)
Mtu anayehubiri uchafu (mienendo mibovu ya kimaisha) huyo ni tapeli. Mhubiri ambaye maisha yake hayaoani na kile anachokihubiri cha kweli katika neno la Mungu, huyo ni tapeli pia. Muepuke.
6. UPENDO.
(Mathayo 22:37-38, 1Yohana 4:7, 1wakorintho 13:9)
Mungu ni upendo, Yesu ni upendo, Injili ni upendo na ukristo halisi ni Upendo. Hakuna upendo hakuna ukristo.
Mhubiri anayehubiri chuki, choyo, ubinafsi ni tapeli wa kiimani. Mfano Mhubiri anayejivunia ukwasi alionao huku akishindwa kuumia kuona umaskini wa watu wanaomzunguka katika maisha yake ya kila siku, huyo ni tapeli tu.
Mhubiri au taasisi ya kikristo ambaye/ambayo haiumii au inashindwa kuchukua hatua madhubuti za kutatua baada kuona shida za watu wengine (hususani wasio waumini wa imani hiyo) katika jamii yake, huyo mhubiri/taasisi ni utapeli chini ya mwamvuli wa ukristo. Ukristo sio kujazana makanisani ili kuimba, kuomba na kufarijiana huku ukipuuzia mengine yanayoendelea kwenye jamii zetu. Ukristo ni ufalme unaotamani kutamalaki kwenye maisha yetu yote ya kila siku.