Jifunze namna ya kutengenza Mkaa kwa kutumia takataka za shambani

Jifunze namna ya kutengenza Mkaa kwa kutumia takataka za shambani

Mkuu unaweza kuelezea kidogo drier mlizonazo zimetengenezwa wapi na zinafanyaje kazi?
Kiufupi kampuni yetu inajihusisha na manufacturing/fabrication and design of several machine, hizi drier tunatengeneza wenyewe. Briquette(mkaa) huwa unasafiri (by chain conveyor) katika closed line ambayo iko indirect contact na heat ambayo inazalishwa na hayo mafuta machafu. Ni rahisi na iko efficiently, yani mkaa ukitoka hapo unapack katika mifuko tayari kwenda sokoni.
 
Kaka kama unaweza naomba utupe Jina la kampuni yenu,anwani na bei ya hiyo dryer.Ilikuwa nianze hii kazi ya kutengeneza mkaa sema nikwa na changamoto sehemu ya kuanika coz eneo hakuna.
Na je hiyo drier ndio pia machine ya kutengeneza mkaa au yenyewe ina kausha peke yake.
Asante sana na Ubarikiwe
 
Salaama mkuu..drier ni ya kukaushia tu. haitengenezi mkaa.
 
Salaama mkuu..drier ni ya kukaushia tu. haitengenezi mkaa.

Asante ila hujatupa jina la kampuni yenu na mawasiliano ya jinsi ya kuwapata.Mimi nahitaji hiyo drier seriously kama itakuwa sio garama kubwa sana
Tafadhali naomba nijuze jinsi ya kuwapata
 
Ndugu dikembe, bado mnazo hizo mashine za kutengeneza briquettes? Kama zipo, tafadhali taja namba za simu, na mnapopatikana
 
Hello JF members!

Natoa shukrani za dhati kwa hili jukwaa. Ni kwa namna nyingi nimenufaika nalo.

kwa wale wanaotaka kujifunza kutengeneza mkaa nimewaanzishia huu uzi. Najua wapo walioamua kuuza huu ujuzi kwa namna mbali mbali. hapa naanika bure kile nikijuacho.

Furahia na tengeneza hela!

KUTENGENEZA MKAA KWA NAMNA RAHISI.
Mahitaji:
1.Takataka za mashambani: magunzi, mbaki ya kuangua nazi, majani, makuti ya mmnazi na kadhalika. Au vumbi la mkaa uliosalia kwenye uuzaji au tanuru la kuchomea mkaa
2. Chombo cha kuchoma takataka za mashambani. Drum bovu, ndoo la chuma au kinginecho
3. Bomba la plastiki la nchi tatu upana urefu nchi sita
4. Mche wa kugandamiza
5. Unga mchafu, pumba zilizosagwa au mckanganyiko wa karatasi laini na na maji(paper pulp) ambao utatumika kama gundi.

HATUA YA KWANZA.
Kubadili taka kuwa hali ya mkaa (carbonisation process)
kusanya takataka za mashambani kisha weka kwenye drum (liwe na matundu madogo chini halafu zichome. Zikiwaka baada ya moto mkali kutulia weka mfuniko kisha pembezoni ziba na tope(udongo na maji) ili hewa isiingie. Acha kwa muda mpaka taka zigeuke kuwa mkaa. Mimina na acha mkaa upoe.
C:\Users\Ariela\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.png

HATUA YA PILI.
Twanga mkaa ili kupata unga kama unavyoonekana hapo chini. Kama ni mabaki ya mkaa twanga na chekecha kupata unga

C:\Users\Ariela\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image004.jpg

HATUA YA TATU
Kuandaa gundi ya mkaa. Chukua unga ( unawaza kuwa wa muhogo, mahindi, ndizi (pia maganda ya nafaka hizi yanafaa, pumba n.k ) au nafaka nyingineyo. Vipimo ni nusu kilo ya unga itatumika kuchanganye na kilo kumi ya vumbi ya mkaa. Chukua unga upike uji mzito kabla ya kuchanganya na mkaa kama inavyoonekana hapo juu kwenye picha. Uji wakati unachemka ukianza kutokota utakuwa tayari. Changanya ukiwa wa moto na finyanga uwe kama ugali.
Angalizo: usifwate sana vipimo. Aina ya taka zina vumbi la aina tofauti. Unaweza ukalowanisha vumbi lako la mkaa kwanza kabla ya kuweka gundi (binder) pia ukiona wakati unachanganya ni mlaini sana ongeza vumbi. Ukiona ni mgumu sana ongeza uji (gundi) finyanga kama ugali.
HATUA YA NNE
Uzalishaji: unaweza ukafinyanga matonge kwa mkono na kuweka juani yakauke. Pia unaweza kutumia njia hii rahisi
Utahitaji

  1. bomba la plastiki nchi 2 mpaka nchi 3 kwa kipenyo na nchi 4 mpaka 6 kwa urefu
  2. Mche wa kusukumia (kugandamiza) hakikisha unateremka kwa urahisi kwenye bomba (usibane wala kukwangua)
  3. Kibao cha kuweka chini
C:\Users\Ariela\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image005.png

Weka mkaa ndani ya bomba kisha gandamiza (unaweza kugonga na mbao kidogo kwa juu kama bomba lako ni gumu vya kutosha unaweza kutumia la chuma pia kwa kazi hii) geuza upande ulioshikia na gandamiza kutoa mkaa. Mche ukae kwa chini na wewe ukamate bomba mkaa upande juu.
C:\Users\Ariela\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image006.png

HATUA YA MWISHO
Anika mkaa wako kwenye jua kwa siku nne hadi tano. Tumia ukiwa umekauka sawasawa.
Mwisho kabisa
Mwongozo huu ni kukuwezesha kujua machache. Nitazidi kuboresha hii post. Kwa makosa ya uandishi kazi hii nawaachia editors.
Asante sana mkuu maana nilikuwa nimeazimia kufanya mradi huu punde baada ya kumaliza kusoma uzi huu
 
Kiufupi kampuni yetu inajihusisha na manufacturing/fabrication and design of several machine, hizi drier tunatengeneza wenyewe. Briquette(mkaa) huwa unasafiri (by chain conveyor) katika closed line ambayo iko indirect contact na heat ambayo inazalishwa na hayo mafuta machafu. Ni rahisi na iko efficiently, yani mkaa ukitoka hapo unapack katika mifuko tayari kwenda sokoni.
Bei ni kiasi gani mkuu
 
Back
Top Bottom