Jifunze QGIS

Jifunze QGIS

QGISInsights

Member
Joined
Apr 26, 2023
Posts
16
Reaction score
41
Habari wakuu!

QGIS ni programu ya bure. Jina QGIS linamaanisha "Quantum GIS" na awali ilianza kama mradi wa Quantum GIS mnamo mwaka 2002. QGIS ni program bora sana kulinganisha na program zingine. Pia ni program rahisi sana kujifunza na kuitumia!

Nitatumia ukurasa huu mara kwa mara kuandika na kutuma video kadhaa za mafunzo ya jinsi ya kuitumia.

Kuna faida kadhaa za kutumia QGIS. Hapa chini ni baadhi ya faida hizo:

1. QGIS ni programu ya bure , hivyo unaweza kuitumia bila gharama yoyote

2. QGIS inatoa uwezo wa kufanya kazi na aina mbalimbali za data ya ramani (data types), ikiwa ni pamoja na data ya raster, data ya vector, na data ya tabular.

3. QGIS ina zana mbalimbali za uchambuzi wa data za GIS, ambazo zinaweza kutumiwa kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kijiografia, kufanya hesabu, na kupata taarifa za ziada.

4. QGIS ina zana mbalimbali za kujenga na kuhariri ramani za GIS, ambazo zinaweza kutumiwa kwa ajili ya kujenga ramani za kitaalamu kwa urahisi.

5. QGIS ina Plugins nyingi za kuboresha uwezo wa programu, ambazo zinaweza kutumiwa kwa ajili ya kuongeza uwezo wa programu kama vile zana za uchambuzi wa ziada.

Karibuni.
 
Mkuu ni kwa namna gan naweza fanya soil analysis kupitia Qgis
 
Mkuu ni kwa namna gan naweza fanya soil analysis kupitia Qgis
Kiongozi, nimechelewa kuona reply sikujua kama uzi wangu umesharuhusiwa kuwa hewani. Yes inawezekana kufanya Soil Analysis kupitia QGIS! Je, una sample data zozote za udongo wako zenye coordinates za eneo umechukua? sample data ziwe na taarifa kama pH, nutrients etc.. Ukiwa nazo, then naweka somo hapa step by step!
 
Ahsante Sana.., Hapa kwenye kuonyesha hizi pH na parameters nyingine maana yake utachora ramani yenye points na kuweka rangi kuonyesha status Kwa kila parameter?
 
Back
Top Bottom