Tuweke jambo sawa kidogo hapa. Katika sarufi (grammar) wakati (time) si sawa na njeo (tense). Wakati (time) ndiyo hugawanyika mara tatu, yani, uliopita, uliopo na ujao lakini njeo (tense) ni lile umbo la kitenzi(verb) ambalo hujidhihirisha kwa namna mbili kuu, umbo linaloonesha wakati wa sasa na lile la wakati uliopita.Tukichambua maumbo haya kwa kila muktadha, yani , uliopo ama uliopita, tutapata maumbo tofautitofauti kadiri mzungumzaji anavyotaka kuwasiliana. Hivyo, neno TALK linaweza kuwa talked, talking ,talk(s) n.k.
Kumbuka hali ya kitenzi kuwa katika wakati uliopita ama wa sasa haina uhusiano wa moja kwa moja na wakati(TIME).Tazama mifano ifuatayo:
If I were a woman, I could bear children.(Je, unadhani huu ni wakati gani, uliopita ama wa sasa? Je, hizo tense ni wakati gani, were/could?) Tazama mfano unaofuata:
Could you give me a pen? (Unadhani huu ni wakati gani, tensi gani?, Je nikikwambia hivi maana yake ninakwambia jambo lililopita? Hapana hii ni sasa, present lakini kitenzi cha wakati uliopita.
Kwa kifupi, katika mifano yote hiyo hapo juu vitenzi vinaonesha wakati uliopita lakini lakini wakati ni wa sasa hivi.
Kwa minaajili hii, Kiingereza hakina umbo maalumu kuashiria future tense. Wengine husema hakina future tense, bali kina wakati ujao tu. Waingereza wao hutumia tense mbalimbali kueleza masuala ya wakati ujao. Tazama mifano michache hapa chini:
1. I am going to marry her next week.(going to)
2.I will go to school on Saturday.(will)
3.Exams start this weekend.(present tense)
4. I am about to finish my studies.(about to)
5. I am visiting my mum this evening.(present continuous)
Mifano hii inathibitisha kuwa hakuna umbo maalumu kudhihirisha future tense katika English. Na hii inathibitisha tense si sawa na time(wakati), kwani utaona hapo present tense imetumika kuelezea masuala ya wakati ujao na kule mwanzoni tuliona maumbo ya wakati uliopita yametumika kueleza matukio ya present time.
Mkanganyiko huu unatusumbua sana sisi ambao tunajifunza Kiingereza kama lugha ya pili. Na ukisoma kw akuchambua kama hivi, ndiyo unachanganyikiwa kabisa. Usomaji mzuri ni ule wa kupewa muktadha(context) , kisha unapewa kanuni indirectly na kuoanisha na muktadha uliopewa. Kwa mfano, unataka kujifunza wakati ujao, utapewa kisa cha Jolita anataka kuoa mwakani. Utawasikiliza kisha utaona miundo wanayotumia na wewe kuweza kuiga huku mwalimu akisiriba kwa kanuni.
Ninawasilisha