IV.Present perfect continuous tense
View attachment 1107761
Tumeshasoma tayari " present perfect tense " . Sasa leo tuangalie " The present perfect continuous tense " .
Present perfect continuous tense - nyakati hii hutumika kuonyesha vitendo ambavyo vipo katika hali timilifu inayoendelea ( Yani
kitendo kilikuwa kimefanyika lakini katika hali ya kuendelea ) .
JINSI YA KUTENGENEZA SENTENSI ZA " PRESENT CONTINUOS TENSE " .
1.
Kwa sentensi za kukubali / chanya
SUBJECT + HAS / HAVE + BEEN + MAIN VERB + ING
Ufafanuzi
MAIN VERB - Hiki ni kitenzi kikuu , kitenzi hiki tunaongeza ING mbele . Mfano : live / living , go / going , see / seing .
"
Have " inatumika na I , You , We na They ( Nafsi ya kwanza umoja , na nafsi zingine isipokuwa nafsi ya tatu umoja )
"
Has " inatumika na He , She na It.
Mfano :
I have been living here for 2 years
( Nimekuwa nikiishi hapa kwa miaka miwili ) .
She has been working here for 4 months .
( Amefanya kazi hapa kwa miezi minne )
2.
Kwa sentensi za kukanusha / hasi
SUBJECT + HAS / HAVE + NOT + MAIN VERB + ING
Mfano : I have not been ......
3.
Kwa sentensi za kuuliza maswali
HAS / HAVE + SUBJECT + MAIN VERB + ING
Mfano : Have you been.......
MIFANO ZAIDI .
I have been waiting for you 4 hours .
( Nimekuwa nikikusubiri kwa masaa
manne )
I'm tired because I have been running .
( Nimechoka kwa sababu nimekuwa
nikikimbia )
You have been talking to him since
morning .
( Umekuwa ukiongea nae tangu asubuhi )
It has not been raining.
( Haikuwa ikinyesha )
We have not been playing football .
( Hatukuwa tukicheza mpira )
You don't understand now because you
have not been listening
( huelewi sasa kwa sababu haukuwa
ukisikiliza .)
Have they been doing this work ?
( je , wamekuwa wakifanya kazi hii )
***************************