Jifunze Ubahili, itakusaidia kuepuka matumizi ya pesa ovyo

SaveTheOthers

Member
Joined
Jan 29, 2017
Posts
99
Reaction score
232
Wasalaam Wakuu.

Ubahili ni moja ya nguzo muhimu Sana katika kufanikiwa. Ni hali ya kuwa na nidhamu ya fedha kwa kujibana au kutafuta njia za kupunguza gharama zisizo na msingi. Lengo kuu hasa la ubahili ni ku-save na ukishakuwa na savings za kutosha, bila shaka maisha yataenda vema.

Naomba Leo tujifunze jinsi ya kufanya ubahili.

KWENYE USAFIRI.
Hakikisha kuwa chenji yako yote inarudishwa. No keep change. Kama Nauli ni Tsh 450, ukitoa 500 basi hakikisha kuwa unarudishiwa 50 yako. Hii itakusaidia kutokupuuza gharama ndogo ndogo. Every cent counts in. Hizo hamsini ukizichukua na kuzipeleka kuweka kwenye kibubu, huwezi amini kuja kuipasua ni fedha nyingi sana na hapo ndipo utakapoelewa ni kiasi gani cha fedha ungepoteza kwa kupuuzia hizo Tsh 50.

Kama una option ya kusafiri na ndege au bus basi jifikirishe vizuri. Ndege gharama zake ni nyingi mno. Kama hakuna unachokiwahi, huna haja ya kutumia usafiri wa ndege. Enenda na bus na kilichobaki itunze.

KWA WANYWAJI.
Kama wewe si mtumiaji wa vilevi, hakikisha unachonunua hakikuumizi. Mfano, kuna grand Malta za Kopo (2000) na ya chupa (1000) na zote zina ujazo sawa na ubora ule ule. Hakuna haja ya kutumia elfu mbili wakati kuna bidhaa ya Tsh 1000 sema tatizo ni packaging. Save hiyo 1000 ya ziada.

Kwa wanywaji wa pombe. First rule, kwa mabahili ni "NO KEEP CHANGE". Chukua hata kama imebaki 200, Chomeka mfukoni. Fika nyumbani tupia mezani, kesho itafanya kazi nyingine.

Pia, hakuna haja ya kwenda kunywa bia yenye ladha ile ile na ujazo ule ule iliyotengenezwa na kampuni moja inayouzwa kwa Tsh 3000 wakati mwenzako anakunywa kwa Tsh 1500. Hayo ni matumizi mabaya ya fedha. Save money for the future.

JUU YA MAVAZI.
Kuna nguo ukienda Tandika unaipata kwa Tsh 13,000 lakini ukienda Mlimani City unauzia 35,000 with no discount kwa brand na label ile ile . Yaani, ndiyo kusema 22,000 yote imeenda na maji. Vaa nguo pendeza, tumia gharama ndogo.

MENGINEYO.
Kama umeenda sokoni, ulizia punguzo kwa kila utakachonunua. Siyo unaambiwa nyanya 1500 kwa fungu, wewe unatoa tu. Omba kupunguziwa, pengine hizo nyanya ni Tsh 1000 tu. Sasa wewe umepoteza 500 yote kwa kujidai.

NO SHOW LiFe kwa mabahili. Usitake kujionyesha kuwa maisha yako ni mazuri. Kwa kufanya hivyo utashindwa kujibahili na kuanza kufanya matumizi yasiyo na msingi. Ishi maisha yako. Utawanyoosha uzeeni.

MENGINEYO.
Nunua kwa bajeti. Siyo unajaza vitu ndani huvitumii. Vinakaa ndani mpaka vinaharibika, kufanya hivyo unalazimisha matumizi mengine ya fedha yasiyo na msingi ya kununua vitu upya.

Usiwashe TV kama hakuna ishu ya maana ya kuangalia. Washa kipindi cha taarifa ya Habari tu. Itakuounguzia gharama za umeme.

Taa zisizo na msaada wakati umelala nazo zizimwe. Itasave bill ya Umeme.

Maji pia yatumike ipasavyo.

LINGINE.
Ukienda kwenye manunuzi, andaa bajeti kabisa. Siyo unaenda na kuanza kununua ovyo. Pia, usibebe kiasi kikubwa cha fedha. Kama manunuzi ulipanga yawe 25,000 basi beba 35,000. Hiyo 10,000 itakuwa ya emergency. Kubeba fedha nyingi zitakuwasha na kuanza kufakamia matumizi ambayo hukuyatarajia.

Mengine wataongezea Wakuu.
 
Nilikuwa nasubiri ushauri kwenye kuhonga
 
Back
Top Bottom