Jihadhali na matapeli hawa hapa

Jihadhali na matapeli hawa hapa

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Leo saa 10:11 jioni nimetumiwa meseji ya kitapeli kutoka namba +255684475742. Meseji inasomeka hivi:

+15092142532: Your Mobile No has won 1,000,000 Dollars in Coca Cola USA, to claim send your name, address, work, age, phone No, to Dr. Robert Email: cocacola.us@live.com

TAHADHARI
1. Wakuu tuchukue tahadhari kuepuka mitego ya hawa matapeli. Baada ya mbinu zao za kale kushindwa, naona wameamua kuja na mbinu mpya na mbaya zaidi.

2. Vyombo vya usalama vinapaswa kuchukua hatua kuwafuatilia na kuwakamata matapeli hawa ili raia wasiendelee kutapeliwa na hawa majizi kwani sio watu wote wenye uelewa wa kuwakwepa hawa wanaharamu.

3. Kampuni ya Airtel inapaswa kuwafuatilia hawa matapeli kwa njia ya mtandao na kubaini mahali walipo ili polisi wawasake na kuwatia nguvuni. Ni wazi kwamba namba za simu siku hizi zinarekodiwa, kwa hiyo itakuwa rahisi kujua namba hii inamilikiwa na nani ili asakwe, akamatwe na kutiwa adabu ya kisheria. Isije tena ikawa kama ile kesi ya Prof Kapuya aliyedai kugawa laini yake kwa mtu mwingine wakati imesajiliwa kwa jina lake! Hata kama namba imegawiwa kwa mtu mwingine, aliyeisaijili ndiye atakayewajibika kwa uhalifu wowote utakaotendwa kwa kutumia hiyo laini. Mshikwa na ngozi ndiye mwizi, au sio?

Natumaini kwamba kila mtu (serikali, wananchi na vyombo vya usalama) atacheza nafasi yake ili kutokomeza uhalifu huu wa kimtandao (cybercrime) na kuwafanya raia waishi kwa amani na furaha.

Nawasilisha
 
..mi nimewahi tumiwa mesage kama miaka minne iliyopita lakini yenyewe jamaa walikuwa wanajifanya ni kampuni ya nokia na wakati huohuo na mimi nilikuwa natumia simu ya nokia.
ilikuwa ni rahisi wa wakati ule lakini kwa kiwango kile cha pounds

baada ya kuanza kufatilia website waliyoitoa nikakuta ni ya kitapeli

so huu utapeli wa aina hii haujaanza leo.
 
Taarifa ni nzuri Ifanyiwe kazi kudhibiti majizi hayo ya kimtandao.
 
Watamzania tunategeka na mitego hii na wale telexfree kwa kuwa tunapenda miteremko
 
Doh nashukuru kwa taarifa hii nayo mpya ingenikuta mimi doh ningeibiwa
 
Ukiwa a bit cautious a bit smart hutotapeliwa kirahisi
 
Wabongo msimuamini kila mtu au kila kitu, Wanaijeria wamejaa hapa nchini,
 
Facebook ndo wapo wengi,ila najiuliza huwa facebook admins wanawagunduaje hawa jamaa,yaani ukiamka unakuta wameshawablock
 
Mi walinitumia nikadelete uchafu wao,baada ya muda wakatuma tena nikaipotezea tena kwa namba hiyohiyo! ila nachojua nchi yetu ina mifomu ya hovyo sana..iko kwenye maandishi tu ila effectiveness zero.jaribu kuulizia TCRA ishu yoyote uone wanavyozingua!
 
Hawa matapeli wanaendelea jana nimetumiwa message toka namba+255689667392 ikiwa inasomeka
COCA COLA AWARD: YOU HAVE WON 750,000 DOLLARS iN USA COCA COLA AWARD TO CLAIM SEND U NAME ADRES WORK AGE TO DR. HARRY: coca.cola20141award@usacom +1323060466

Leo tena nimetumiwa sms toka namba +255068786854 inasomeka+1509142532:Your Mobile number Has Won 1,000,000 Dollars in Coca Cola Award USA, to claim send ur Name, Phone No, Age, Address, Job to Robert Email: cocacola.us@live.com


This is a scam, hope TCRA wanafuatilia wamiliki wa hizo namba za airtel
 
waambie wanitumie na mimi hiyo meseji nikajichukulie mihela hiyo.
Nalog off
 
Huwezi ukashinda kiasi chote hicho cha pesa halafu utumiwe msg....achilia mbali kama ulicheza au la
 
Hivi in case ukiwatumia adress yako na jina kama wanavyotaka..watafanya nini next?
 
Back
Top Bottom