Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi in case ukiwatumia adress yako na jina kama wanavyotaka..watafanya nini next?
kwanini usijaribu mwenyewe mkuu ukapata jibu la uhakika
Leo saa 10:11 jioni nimetumiwa meseji ya kitapeli kutoka namba +255684475742. Meseji inasomeka hivi:
+15092142532: Your Mobile No has won 1,000,000 Dollars in Coca Cola USA, to claim send your name, address, work, age, phone No, to Dr. Robert Email: cocacola.us@live.com
TAHADHARI
1. Wakuu tuchukue tahadhari kuepuka mitego ya hawa matapeli. Baada ya mbinu zao za kale kushindwa, naona wameamua kuja na mbinu mpya na mbaya zaidi.
2. Vyombo vya usalama vinapaswa kuchukua hatua kuwafuatilia na kuwakamata matapeli hawa ili raia wasiendelee kutapeliwa na hawa majizi kwani sio watu wote wenye uelewa wa kuwakwepa hawa wanaharamu.
3. Kampuni ya Airtel inapaswa kuwafuatilia hawa matapeli kwa njia ya mtandao na kubaini mahali walipo ili polisi wawasake na kuwatia nguvuni. Ni wazi kwamba namba za simu siku hizi zinarekodiwa, kwa hiyo itakuwa rahisi kujua namba hii inamilikiwa na nani ili asakwe, akamatwe na kutiwa adabu ya kisheria. Isije tena ikawa kama ile kesi ya Prof Kapuya aliyedai kugawa laini yake kwa mtu mwingine wakati imesajiliwa kwa jina lake! Hata kama namba imegawiwa kwa mtu mwingine, aliyeisaijili ndiye atakayewajibika kwa uhalifu wowote utakaotendwa kwa kutumia hiyo laini. Mshikwa na ngozi ndiye mwizi, au sio?
Natumaini kwamba kila mtu (serikali, wananchi na vyombo vya usalama) atacheza nafasi yake ili kutokomeza uhalifu huu wa kimtandao (cybercrime) na kuwafanya raia waishi kwa amani na furaha.
Nawasilisha
mimi waliwahi kunitumia hiyo email wakaomba account no nikawatumia account ya OC ya mkurugenz wa halmashauri yetu sasa sijui waliiba watajua wenyewe