Jihadhari dhidi ya hao unaowatambulisha kwa bosi wako kwani kesho ndio watarudi kimya kimya kukuchoma

Jihadhari dhidi ya hao unaowatambulisha kwa bosi wako kwani kesho ndio watarudi kimya kimya kukuchoma

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
471
Reaction score
1,217
Ubinadamu haupo kwa kila mtu kuna wengine kimaumbile ni watu lakini ndani ni wanyama wakatili sana pengine zaidi hata ya hao wanyama mwitu.

Ukilitambua hilo utakuwa makini sana kwa sababu furaha yako itamaliza na mtu ambaye ulitarajia mazuri kwake .

Leo hii unaweza kutumia mtumbwi wako kumvusha mtu mtoni lakini baadaye hurudi kuutoboa kama shukrani.

Unaweza muonyesha mtu Ng'ombe akupaye maziwa na tena ukampa mpaka maziwa anywe lakini kesho ndio anakuwa wa kwanza kupanga njama za kumpa sumu kama shukrani.

Kuna muda unaweza kujuta kuwa mwema kwa sababu uliyemfanyia hakuwa na ubinadamu ndani yake .

Unaamua kumbeba mtu lakini anakukojolea kichwani kama shukrani.

Katika haya maisha jiwekee ulinzi pia usiwe mwepesi sana kuwaonyesha watu kinachokupa furaha kwani hawakawii kuja kuvuruga, Kila siku kuwa mtu wa tahadhari na mipaka .

#Mwanasayansi Saul kalivubha
 
Kweli Leo nimepokea taarifa njema kuhusu maswala yangu Fulani,nikaona nimshirikishe ndugu yangu ambaye kaniZidi kila kitu.

Lakini reactions zake zimenitafakarisha sana inaonesha huwa hafurahii jitihada zangu picha ya kunizidi kila kitu.
 
Pole sana ndugu
 
Back
Top Bottom