Jihadhari na matapeli hawa wa Kupatana.com

Jihadhari na matapeli hawa wa Kupatana.com

Habari ya wakati na muda kama huu ndugu zangu watanzania na East Afrika kwa ujumla. Nianze kwa kutoa pole kwa ndugu jamaa na rafiki wote walioko kwenye mfungo. Mwenyezi awajalie wepesi.

Dhumuni la kuanzisha thread hii ni kuwafungua tu macho watu hasa wale wanaopenda biashara ya mtandao. Kuna mitandao mingi sana ila leo naomba tuongee hii site ambayo ni kama "advertising center" www.kupatana.com

Kwa mimi kupatana ndio kama kariakoo yangu na nina uzoefu sana na pia ninmara chache sana inatokea nafanyiwa dhuluma na hii ni pale mtu anaamua kukuuzia kitu kwa ujanja ujanja ila pia mwisho wa siku ukitumia mbinu mbadala anapatikana.

Kuna siku niliingia kupatana nikakutana na tangazo hili

8a8a036801f473973d4e0221d631c4fc.jpg

dcf6558116283d017ca2e8de9d3bdf80.jpg

Nilipoona tangazo ninla bei rahisi na namba iko ya nchini kwetu kwanza nikapiga, haikuwa hewani ndipo nikamchatisha whats app
Mazungumzo yalikua hivi

705a3cf2b27554ff3fc82681e1efc220.jpg

Akaniambia yuko kenya na kujitetea kwingi. Sasa uzuri mimi kenya ni kama nyumbani. Nina marafiki kibao na ndugu pia nikaona sio kesi nikaunda Group kati yangu mimi, yeye na Derick rafiki yangu aloko kenya

2c00af1eb7ad5c642f84e222122faa17.jpg

Jamaa akawa analefu tuu kila saa ikabidi nimfate inbox nimtulize wenge kwa kumuelewesha

3d1e8ca505291b4b6a5e98061ffdddcf.jpg

Hatimaye akakubali kua kwenye group nikamrudisha tena na mazungumzo yakaendelea kama ifuatavyo

2a1e0ce7e356a238c6cd5be3ec4fe825.jpg

14f276813569ae9852d79abf34ea9e19.jpg

Nilivoona anataka biashara za yule jamaa mwingine anaesemaga yuko mtwara nikamuuliza jina la kampuni labda ingenipa muongozo

52b3b0e61e309a07985403a5721becd2.jpg

Baada ya kutaja jina la kampuni niliingia Google na kuangalia cha kwanza nikakuta kampuni iko india. Sikutilia maanani kwani majina tu yanaweza kufanana ila nikafanya more digging sijakuta kampuni yenye jina hilo kenya

f89888fb985298859fe795a2629efd25.jpg

Baada ya kukosa kampuni hio ilinipasa kuomba blog au website pengine hapo ningepata mwanga. Aliposema pia hata hivo hana nikajua hawa ndo walewale wanasubiri watu watafute pesa kwa jasho wao waje wale kirahisi.

b738806ce6707e96aa20535fed5ebb02.jpg

Ombi na pendekezo langu si kwa wamiliki wa kupatana tuu, bali humu jamii forum (matangazo madogo madogo) na hata kina OLX muwe na acccess ya kumwezesha mtumiaji wa hii service yenu kulalamika pale anapofanyiwa fraud, mkiridhika na utafiti kwamba kweli mlengwa au mtajwa ametapeli basi muwezeshe kutiwa nguvuni kwa jangiri hilo.
Najua mnaogopa kupoteza viewers kwa ajili ya CPM na mambo kama hayo, ila ukiangalia kwa undani watu wengi watakua wanatumia mtandao wako kwani wana uhakika walau asilimia 60% kwamba hata wakipigwa (kutapeliwa) kuna msaada.
NI HAYO TUU WAKUU KARIBUNI KWA KUCHANGIA
Umetufumbua macho Ahsante sana mkuu
 
Kupatana ukiona namba yyt ya nje, kaa mbali huyo n tapeli wa moja kwa moja, yote hayo uliyosema mkuu mm nilishayapataga, sema yy alikua Uganda, akalazmisha nitoe pesa nusu halaf nisubirie mzigo ufke nimalizie, yy nilimuuliza swali rhc tuu km anitajie tawi lao hapa bongo, aliishia kung'aa sharub, hata haikua ngumu kujua n tapelii.

Kitu kingne tusizid kupenda kitonga/ mfuko wa shati, jitu linaona s8 plus inauzwa lak 8, nalo linaaamin, lazma ulizwe
4ab33d9b908b34b1ab7b5e0b13314fd3.jpg
54f9fe467c3787e075241dc7015cfe93.jpg
 
Yaani hii sim labda mtu awe amenunua alafu shida imemshika sehemu nyeti ndo atauza bei kama hio. Sasa hapo kwa laki nane wazaramo wa kizungu wanasema "too good to be true"
 
Hawa watu wamefika Facebook sasa wanawaambia watu wanaweka channel za dstv kwenye vingamuzi local kama startimes na Azam. Ukituma ela umeisha
 
Hawa watu wamefika Facebook sasa wanawaambia watu wanaweka channel za dstv kwenye vingamuzi local kama startimes na Azam. Ukituma ela umeisha
Yaani hata king'amuzi kipo nyumbani kwako unalipia juu kwa juu? Au wanakwambia wanakurekebishia wakiwa hukohuko...

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Yaani hata king'amuzi kipo nyumbani kwako unalipia juu kwa juu? Au wanakwambia wanakurekebishia wakiwa hukohuko...

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
Wanakuambia uwatumie hela uone chanel za DSTv kwenye startimes. Sasa kutokana na ugumu wa maisha naona watu wanaona inaweza ikawa kweli au wanajitia uvivu wa kufukiria wanaishia kueka mikono kichwan.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliuziwa htc one m8 kwa 400k .niliumia sanaaa. Nilikuja kushtuka kumbe simu ina tatzo la soft ware. Na fake pia.

Nilichofanya niliamua kupambana na simu yangu na mimi nikawa mwanaume wa mjini nilifanya yangu namimi nkamuingiza mtu mjini kwa exchange deal....matako yako rajabu ulieniuzia simu fake ila nimejifunza na sitokaa nitapeliwe tena kupatana...

sent from my iPhone 7s using JamiiForum mobile app.
 
Kupatana kuna wauzaji legit wapigaji na ambao wako kotekote. Unakuta mtu mlikua mpige deal legit ila akishakuona akakusoma anabadili upepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom