Jihadhari na Upatu, ukidhurumiwa hutopata haki yako

Jihadhari na Upatu, ukidhurumiwa hutopata haki yako

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
234
Reaction score
376
JIHADHARI NA UPATU, UKIDHURUMIWA HUTOPATA HAKI YAKO.

Siku hizi limeibuka wimbi kubwa la watu wanaojifanya kuanzisha na kuendesha mpango wa uwekezaji wenye faida kubwa huku wakitumia ushawishi kuwarubuni wengine wajiunge katika mpango huo wanaounadi kwamba ni uwekezaji wenye faida kubwa ndani ya muda mfupi. Huu unaitwa mpango wa piramidi (pyramid schemes) au upatu.

Upatu ni mpango wa kuchangisha fedha unaoendeshwa na mtu au kikundi fulani cha watu kwa ahadi ya kuwapatia wachangiaji kiasi kikubwa cha faida ndani ya kipindi kifupi.

Pamoja na madhara yatokanayo na upatu lakini watu wengi wamejikuta wakikubali kurubuniwa na waendeshaji wa mpango huu kwa kuaminishwa kwamba wanaweza kupata faida kubwa sana ndani ya kipindi kifupi kupitia uwekezaji ambao wanaufanya kwa kuwapa fedha hao waendeshaji huku wao wakitulia na kusubiri matokeo au faida ya uwekezaji wanaominishwa kuufanya.

Sijui niseme ni uvivu wa kufikiri au ni mbinu kali wanazotumia!! lakini ukweli ni kwamba watu wanaorubuniwa ni wengi mno na huwa wanashawishika zaidi kujiunga kutokana na mambo kama hayo yafuatayo;
(1) Kutaka kupata faida kubwa ndani ya muda mfupi.

(2) Kutaka kupata fedha bila wao wenyewe kujishughurisha na chochote.
au
(3) Tamaa ya kupata utajiri wa haraka.

Siku zote waendeshaji wamekuwa wajanja sana kwa kuwa na desturi ya kuwaonesha wachangiaji wapya orodha ndefu ya watu mbalimbali na kuonesha mafanikio makubwa waliyopata kama faida kutoka na kushiriki kwao katika shughuri za upatu.

Kwa kuoneshwa orodha hiyo ya uongo, watu wengi wanavutika na kudhani kuwa hii ni fursa mpya ya wao kupata utajiri bila kutumia nguvu huku wakiwa na tumaini la kumiliki majumba makubwa, magari mazuri na biashara za maana.

Mchangiaji husika baada ya kuchangia kiasi fulani cha fedha pia anahitajika kuwashawishi wengine ili wachangie kama yeye ili yeye sasa aweze kupata faida kubwa zaidi bila kujua kuwa anawaingiza wenzake katika kutapeliwa fedha au mali zao. Mwisho wa siku wanapoteza fedha na kuanza kulaumiana, ugomvi na mambo mengine kama hayo.

Sheria zetu hapa nchini Tanzania zinakataza mtu kujihusisha na upatu. Upatu ni haramu, upatu ni kosa la jinai. Mtu au kikundi chochote kinachojihusha na mpango huu kinavunja sheria.

Sheria zinazokataza kujihusisha na upatu hapa nchini ni kama hizi zifuatazo;
1. The Penal Code, [Cap. 16 R. E. 2022] (Kanuni ya Adhabu za Makosa ya Jinai)
Kifungu cha 171A cha Sheria hii kinasema kwamba
"Mtu ambaye anaongoza au anasimamia mpango wa piramidi atakuwa ametenda kosa."

Mpango wa piramidi ndio huu upatu haramu unaoelezewa katika makala hii.

Ni kosa la jinai kuendesha, kushawishi watu kushiriki na kushiriki au kuchangia fedha kama upatu haramu. Hivyo anayebainika kukiuka sheria hii atawajibika kwa mujibu wa sheria kulipa faini ya takribani shilingi milioni tano au kutumikia kifungo jela kwa kipindi cha miaka mitano.

2. The Gaming Act, [Cap. 41R.E. 2019]. (Sheria ya Michezo ya Kubahatisha)

Kifungu cha 55(1) kinazuia mtu yoyote kushiriki, kushawishi wengine kushiriki ama kuendesha mpango wa upatu haramu. Kushiriki katika upatu au michezo mingine haramu inayolingana na upatu ni kosa kisheria na adhabu yake ni faini ya shilingi laki tano (Tsh 500,000/=) au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela au vyote kwa pamoja.

3. The Capital Market and Securities Act, [Cap. 79, R.E. 2002] and amendments of 2010.
Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana.
Kifungu cha 131 kinaeleza wazi kwamba, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kutangaza ama kwa kukaribisha au kushawishi umma kushiriki katika uwekezaji au kuchangia mtaji ni lazima aombe kibali cha Mamlaka cha kuweka wazi Waraka wa Matarajio au prospectus na mamlaka itoe idhini ya kufanya hivyo.

Tunapozungumzia Mamlaka, hapa tunamaanisha Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (The Capital Markets and Securities Authority). Mamlaka hii imeanzishwa chini ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana.

Hivyo, mtu yeyote anayaetaka kutoa dhamana au kukaribisha umma kuchangia mtaji ni lazima atoe Walaka wa Matarajio (Prospectus) ambao umeidhinishwa na Mamlaka ya Masoko.

Lakini watu, vikundi au kampuni zinazojihusisha na upatu haramu huwa hawana kibali cha Mamlaka bali wanatumia urubuni kuwaibia watu kwa njia hii ya upatu. Kuna baadhi ya makampuni yamesajiliwa kujihusisha na biashara ya Masoko ya mitaji lakini wanavunja sheria na kujihusisha na upatu haramu kinyume na kibali chao cha biashara.

Ni vyema jamii na nchi kwa ujumla tukachukua tahadhari na hatua stahiki juu ya watu, vikundi au makampuni yanayojihusisha na upatu haramu.

Ukikutana na kadhia hii tafadhali toa taarifa katika vyombo vya usalama kama vile jeshi la polisi au katika mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana. Hatua stahiki zitachujuliwa dhidi yao.

KUMBUKA
Kwako wewe mwananchi mwenzangu, unatakiwa ufahamu kwamba mpango wa piramidi (pyramid schemes) au upatu ni kosa kisheria. Hivyo, ukidhurumiwa hutaweza kudai wala kupata haki Yako. Hakuna haki katika jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Badala yake ukikutwa na hatia ya kushiriki au kushawishi wengine kushiriki katika upatu utachukuliwa hatua Kali za kisheria kwa mujibu wa sheria iliyokukuta na hatia ya kutenda kosa hilo.

Ukijiunga na mpango wa upatu, kwanza kuna uwezekano mkubwa wa kutapeliwa au kuibiwa fedha au mali zako lakini pia utakuwa umevunja sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yako.

Hivyo, kuwa makini sana na hao matapeli wanakufuata inbox huko mitandaoni kama vile katika Facebook, WhatsApp, Instagram na kwingineko au wale anaokuja katika maeneo yako kama vile chuoni, shuleni, mitaani au maeneo ya ibada na kuwaita pembeni kujifanya wanataka kuwapa semina ya ujasiliamali usioleweka kisha kuwataka mtoe fedha za uwekezaji. Ukiona hivyo usikubali na usiwaamini kirahisi utapeli upo kila mahali.

Ndugu msomaji wa makala hii hadi kufikia hapa naamini utakuwa umeelewa vizuri kuhusiana na upatu haramu na madhara yake na kipi unatakiwa kufanya ili usije ukatapeliwa au kukutana na mkono wa sheria.

It's me
A Lawyer and LifeCoach
Mwanasheria na Mwalimu wa maisha.
Jina: Mr George Francis
Simu: 0713736006
Barua pepe: mr.georgefrancis21@gmail.com

Instagram: @george_mwanasheria

Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓
1_1.jpg
 
Waliotapeliwa na kalyanda wanaweza zishtaki media zilizofanya promo ya hio scheme?
 
[emoji685][emoji117][emoji736]KAMA UMEELEWA VIZURI NA UNAHITAJI KUJISAJILI MWENYEWE SASA[emoji736][emoji117][emoji685]

[emoji289][emoji3502][emoji290]WEBSITE[emoji289][emoji3502][emoji290]

BONYEZA LINK hii kujisajili[emoji3502][emoji116][emoji116]



[emoji619][emoji619][emoji619][emoji619][emoji619][emoji619]


Kisha fanya malipo kupata namba ya TOKEN yako sasa[emoji122][emoji122]

Wengine hao[emoji115][emoji115][emoji115]
Mpumbavu mkubwa
 
[emoji685][emoji117][emoji736]KAMA UMEELEWA VIZURI NA UNAHITAJI KUJISAJILI MWENYEWE SASA[emoji736][emoji117][emoji685]

[emoji289][emoji3502][emoji290]WEBSITE[emoji289][emoji3502][emoji290]

BONYEZA LINK hii kujisajili[emoji3502][emoji116][emoji116]



[emoji619][emoji619][emoji619][emoji619][emoji619][emoji619]


Kisha fanya malipo kupata namba ya TOKEN yako sasa[emoji122][emoji122]

Wengine hao[emoji115][emoji115][emoji115]
Wezi hao usikubali
 
Wabongo mnapenda sana mseleleko
 

Attachments

  • 28DA17FB-5E96-497F-83C6-B957113834D2.jpeg
    28DA17FB-5E96-497F-83C6-B957113834D2.jpeg
    61.3 KB · Views: 25
Back
Top Bottom