JIHADHARI NA WIZI WA AJABU MPYA WA SIMU, HASA SIMU JANJA (CELLPHONE)

Jana nilienda kumuona mgonjwa hospital flan hivi ipo mjini kati, sasa mgonjwa akahitaji kitu nikatoka nje nikamletee, ila natoka tu getin natembea kidogo mbele yangu anakuja mwanaume kashika kidaftari, ghafla akaanza kunichekea, mimi nikawa namuangalia tu nimemkazia macho, eti ooh "dada samahani naomba nikuulize", nikampita bado ananisemesha "nakuuliza kitu unisaidie dada angu samahani" mie kimyaaaa,

Pale lango la hospital kuna walinzi teleeee, mbele ya hospital kuna kituo cha polisi, huko kote kashindwa kuuliza aniulize mie mpita njia, mxiiiie.
Ungesoma tu kilochoandikwa kwenye hicho kidaftari sasa hivi ungekuwa polisi unawasaidia kutafuta simu za wadau mbali mbali
 
Iko hivi, anakuja mtu unayemjua vizuri, na wakati mwingine humjui, anakuomba simu unampa; na anaweza kuchukua na ya mwingine, na ya mwingine. Nyote mtampa simu zenu! Manaweza kuuliza kwa nini, au ya nini, huyo mwizi atatoa jibu jepesi, na japo siyo jibu la kuridhisha, mtanyamaza. Akiishachukua, anaondoka. Mnakuja kushtuka baadaye kuwa kawaibia simu. Wizi huu umetokea madukani, kwenye fremu za biashara, ofisini, na msibani. Kwenye eneo moja Kawe, mwizi ametumia mazingira ya msiba kuiba simu zaidi ya kumi wahusika wakiangalia, huku akijihusisha na msiba usiomhusu.
Anawapumbaza akili kimazingaombwe?!
 
Wengine wanauita utapeli, kwa maana simu utaitoa wewe mwenyewe, na inandoka ukiiona.

Iko hivi,
anakuja mtu unayemjua vizuri, na wakati mwingine humjui, anakuomba simu unampa; na anaweza kuchukua na ya mwingine, na ya mwingine. Nyote mtampa simu zenu! Manaweza kuuliza kwa nini, au ya nini, huyo mwizi atatoa jibu jepesi, na japo siyo jibu la kuridhisha, mtanyamaza. Akiishachukua, anaondoka. Mnakuja kushtuka baadaye kuwa kawaibia simu. Wizi huu umetokea madukani, kwenye fremu za biashara, ofisini, na msibani. Kwenye eneo moja Kawe, mwizi ametumia mazingira ya msiba kuiba simu zaidi ya kumi wahusika wakiangalia, huku akijihusisha na msiba usiomhusu.

Katika kimoja kati ya visa vinne vilivyotokea Kawe katika juma moja, mwizi ni msichana anayejulikana alikoiba kwa vile aliwahi kuishi hapo, na anapoishi kwa sasa siyo mbali na eneo la tukio. Aliingia kwenye fremu moja akamuomba dada mmoja simu janja yake akampa. Kiisha akavuka barabara ya mtaa akamuomba mwanamama mwingine simu yake. Alipokuwa amepata simu nyingine akaondoka. Sehemu hiyo ina maduka, magenge, na bucha, na biashara za vyakula sehemu za wazi, na ilikuwa saa za kazi. Hivyo huyo mwanadada alipochukua simu watu walimuona. Wenye simu walipomuona anaondoka wakajaribu kumuita lakini yeye akawa kama anapuuza na kuendelea na safari yake. Na hakuna aliyemkimbiza!

Nilipomhoji mmoja wa walioibiwa kwa nini hawakumfukuza na kupiga kelele akamatwe, alisema waliona vile wanamjua na wanajua kwao wangemfuata nyumbani. Walimfuata baadaye.

Nyumbani mwanadada huyo hakuwa na simu. Simu aliishakabidhi kwa waliomtuma, ikiwa pamoja nay a kwake mwenyewe, na waliomtuma hakuwajua! Na hawakumlipa kitu!

Alipopelekwa polisi ndipo “mchezo” ukagundulika. Kifupi, wahusika walikuwa wanawake wawili waliomwambia karogwa na kwamba wangemponyesha na pia angepata milioni 2. Alipokabidhi simu aliambiwa ili uponyaji ufanye kazi anapoondoka asiangalie nyuma. Alipokuja kuangalia nyuma hakukuta mtu. Aidha mwanadada huyo alipohojiwa ni jinsi gani aliweza kufanikisha wizi huo alisema alielekezwa na wale wanawake kuwa akichukua simu akiulizwa ateme mate chini; na alifanya hivyo. Aidha alieleza kuwa alikuwa pia amepewa kijiwe alichokiweka chini ya ziwa.

Angalizo/Ushauri: Wezi wa namna hii ni vigumu kuwakamata, na anayekamatwa siyo mwizi, ila na yeye katumiwa na kutapeliwa. Wezi wanatumia mambo mawili: Mosi, wanamtumia mtu unayemjua na kumwamini, hivyo ni vigumu kumshutukia haraka. Na hata asipojulikana anaweka mazingira ya kuaminika au udharura. Pili, wanatumia nguvu za giza. Hivyo naona kuna mambo matatu yatakayoweza kutusaidia kukabiliana na wizi wa namna hii:

1. Epuka kupeana simu. Hasa wanawake ndio wenye mtindo huu.

2. Kama una imani ya Mungu, omba wakati wote uwe na Ulinzi Wake. Hii ndiyo naiona kuwa mbinu itakayosaidia wengi, kwa vile wezi wanatumia nguvu za giza.

3. Ukiona mtu anachukuwa simu ya mwenzako nyumbani, kazini, popote; mshtue. Ama, ikiwezekana, mfuatilie mwizi kinyemela hadi anapopeleka simu na kupiga picha. Ikipatikana picha itasaidia kukamata wahusika. Maana inaelekea wezi wanakuwa ni watu wa karibu kiasi cha kujua mazingira na nyendo nyendo za mlengwa. Kwa hiyo picha yao ikipatikana inaweza kuwa rahisi kuwatambua, au hata kuwatafuta kipolisi.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx​
😀😀 huu kusini kawaida sana
 
Duuh sikatai hii imerudi kivingine kuna wale walianza ukisemeshwa na ukajibu umeisha
 
Simu sio kitu Cha kumpa mtu hata Kama ni mke wako hapaswi kupewa simu yako achilia mbali kuiweka charge .

Simu ni office now days watu wanaweka mambo yote ya kiofisi umo then ghafla unampa Mtu simu

Uo sio uchawi ni ukosefu wa umakini katika Mambo yako muhimu mtu hata Kama unamjua akitaka simu anabidi kujieleza Sana sio hivi hivi. Pathetic.
 
Mwenyewe nimeshangaa unampaje mtu simu bila sababu,, yani simu yangu ilivyo na mambo mengi hata mwenyewe tu nikishika nakua makini sana.....
Mimi mtu akiniomba simu lazima nimuulize ya nini, kama ni kumpigia mtu namwambia ataje namba napiga naweka loudspeaker huku nimeishika muongee, au naweza sema sina salio ili mambo yasiwe mengi...
Halafu watu wanapenda kuamini uchawi uchawi, sijui ni ujinga au ndo kutokujiamini🤨🤨
 
😲😲😲 Inafikirisha Sana.
 
Now mjini kuna mambo mengi..
Kumpa mtu nafasi tu tayari kashajua wee wa namna gani na shida huanzia hapo..

Mi huwa straight sana na mambo yangu. Mtu taongea nae kwenye usafiri tuu nje ya hapo hapana.

Na hata huyo wa kwenye usafiri nikiona ana elements za tabia zile mara "nyota yako imefifia"" sijui habari gani ndo mapema hanipati huyo..

Ni bora wakuite muoga mbele ya hao watu aisee. Sometimes hao wajanja wa town wanapigwa sana kutokana na kujiamini.
Unakutana na mtu ile lafudhi yake tuu. Uwezi dhania kama ndo tapeli mwenyewe. Ahaha kumbe sasa.
[emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851][emoji851]
Upo sahihi kabisa, ni bora uwe kauzu kuliko kuongea ongea na watu, mtu akiwa ana shida kabisa hawezi muuliza mpita njia, atauliza vijiwe vya Tax, Bajaji, Boda Boda, Walinzi, Mafundi Viatu hata Polisi sio mbaya kikubwa apate kusaidiwa.
 
Watu wa warumi hawawezi ibiwa simu wale always wanahisi utapekua ukutane na wazee wa sins
 
Wengine wanauita utapeli, kwa maana simu utaitoa wewe mwenyewe, na inandoka ukiiona.

Iko hivi,
anakuja mtu unayemjua vizuri, na wakati mwingine humjui, anakuomba simu unampa; na anaweza kuchukua na ya mwingine, na ya mwingine. Nyote mtampa simu zenu! Manaweza kuuliza kwa nini, au ya nini, huyo mwizi atatoa jibu jepesi, na japo siyo jibu la kuridhisha, mtanyamaza. Akiishachukua, anaondoka. Mnakuja kushtuka baadaye kuwa kawaibia simu. Wizi huu umetokea madukani, kwenye fremu za biashara, ofisini, na msibani. Kwenye eneo moja Kawe, mwizi ametumia mazingira ya msiba kuiba simu zaidi ya kumi wahusika wakiangalia, huku akijihusisha na msiba usiomhusu.

Katika kimoja kati ya visa vinne vilivyotokea Kawe katika juma moja, mwizi ni msichana anayejulikana alikoiba kwa vile aliwahi kuishi hapo, na anapoishi kwa sasa siyo mbali na eneo la tukio. Aliingia kwenye fremu moja akamuomba dada mmoja simu janja yake akampa. Kiisha akavuka barabara ya mtaa akamuomba mwanamama mwingine simu yake. Alipokuwa amepata simu nyingine akaondoka. Sehemu hiyo ina maduka, magenge, na bucha, na biashara za vyakula sehemu za wazi, na ilikuwa saa za kazi. Hivyo huyo mwanadada alipochukua simu watu walimuona. Wenye simu walipomuona anaondoka wakajaribu kumuita lakini yeye akawa kama anapuuza na kuendelea na safari yake. Na hakuna aliyemkimbiza!

Nilipomhoji mmoja wa walioibiwa kwa nini hawakumfukuza na kupiga kelele akamatwe, alisema waliona vile wanamjua na wanajua kwao wangemfuata nyumbani. Walimfuata baadaye.

Nyumbani mwanadada huyo hakuwa na simu. Simu aliishakabidhi kwa waliomtuma, ikiwa pamoja nay a kwake mwenyewe, na waliomtuma hakuwajua! Na hawakumlipa kitu!

Alipopelekwa polisi ndipo “mchezo” ukagundulika. Kifupi, wahusika walikuwa wanawake wawili waliomwambia karogwa na kwamba wangemponyesha na pia angepata milioni 2. Alipokabidhi simu aliambiwa ili uponyaji ufanye kazi anapoondoka asiangalie nyuma. Alipokuja kuangalia nyuma hakukuta mtu. Aidha mwanadada huyo alipohojiwa ni jinsi gani aliweza kufanikisha wizi huo alisema alielekezwa na wale wanawake kuwa akichukua simu akiulizwa ateme mate chini; na alifanya hivyo. Aidha alieleza kuwa alikuwa pia amepewa kijiwe alichokiweka chini ya ziwa.

Angalizo/Ushauri: Wezi wa namna hii ni vigumu kuwakamata, na anayekamatwa siyo mwizi, ila na yeye katumiwa na kutapeliwa. Wezi wanatumia mambo mawili: Mosi, wanamtumia mtu unayemjua na kumwamini, hivyo ni vigumu kumshutukia haraka. Na hata asipojulikana anaweka mazingira ya kuaminika au udharura. Pili, wanatumia nguvu za giza. Hivyo naona kuna mambo matatu yatakayoweza kutusaidia kukabiliana na wizi wa namna hii:

1. Epuka kupeana simu. Hasa wanawake ndio wenye mtindo huu.

2. Kama una imani ya Mungu, omba wakati wote uwe na Ulinzi Wake. Hii ndiyo naiona kuwa mbinu itakayosaidia wengi, kwa vile wezi wanatumia nguvu za giza.

3. Ukiona mtu anachukuwa simu ya mwenzako nyumbani, kazini, popote; mshtue. Ama, ikiwezekana, mfuatilie mwizi kinyemela hadi anapopeleka simu na kupiga picha. Ikipatikana picha itasaidia kukamata wahusika. Maana inaelekea wezi wanakuwa ni watu wa karibu kiasi cha kujua mazingira na nyendo nyendo za mlengwa. Kwa hiyo picha yao ikipatikana inaweza kuwa rahisi kuwatambua, au hata kuwatafuta kipolisi.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx​
Maisha yamekuwa magumu sana!wenye roho nyepesi ndo hao vibaka.
 
Huo ujinga sijaibiwa kwa hiyo style labda itumike nguvu simu ichukuliwe lakini eti naomba simu na mi nimpe big NO
 
Wanaibiwa kizembe sana unampa vipi simu mtu na humjui hadi anaondoka nayo unamuangalia tu. Huu ni uzembe uliopitiliza.
 
Weeeeh!!!
Wanakua wanaandika nini???
Aisee sijawahi kubahatika kusoma, ila kuna watu walishalizwa kiuzembe usikute ni dawa tu ya kukulevya na kupunguza uwezo wako wakufanya maamuzi, daftari ni njia ya kukuvuta karibu ili akuwekee hiyo dawa
 
Mimerudia kusoma mara 2 bado sijakuelewa!
 
Back
Top Bottom