JIHADHARI NA WIZI WA AJABU MPYA WA SIMU, HASA SIMU JANJA (CELLPHONE)

Ungesoma tu kilochoandikwa kwenye hicho kidaftari sasa hivi ungekuwa polisi unawasaidia kutafuta simu za wadau mbali mbali
 
Anawapumbaza akili kimazingaombwe?!
 
😀😀 huu kusini kawaida sana
 
Duuh sikatai hii imerudi kivingine kuna wale walianza ukisemeshwa na ukajibu umeisha
 
Simu sio kitu Cha kumpa mtu hata Kama ni mke wako hapaswi kupewa simu yako achilia mbali kuiweka charge .

Simu ni office now days watu wanaweka mambo yote ya kiofisi umo then ghafla unampa Mtu simu

Uo sio uchawi ni ukosefu wa umakini katika Mambo yako muhimu mtu hata Kama unamjua akitaka simu anabidi kujieleza Sana sio hivi hivi. Pathetic.
 
Mwenyewe nimeshangaa unampaje mtu simu bila sababu,, yani simu yangu ilivyo na mambo mengi hata mwenyewe tu nikishika nakua makini sana.....
Mimi mtu akiniomba simu lazima nimuulize ya nini, kama ni kumpigia mtu namwambia ataje namba napiga naweka loudspeaker huku nimeishika muongee, au naweza sema sina salio ili mambo yasiwe mengi...
Halafu watu wanapenda kuamini uchawi uchawi, sijui ni ujinga au ndo kutokujiamini🤨🤨
 
😲😲😲 Inafikirisha Sana.
 
Upo sahihi kabisa, ni bora uwe kauzu kuliko kuongea ongea na watu, mtu akiwa ana shida kabisa hawezi muuliza mpita njia, atauliza vijiwe vya Tax, Bajaji, Boda Boda, Walinzi, Mafundi Viatu hata Polisi sio mbaya kikubwa apate kusaidiwa.
 
Watu wa warumi hawawezi ibiwa simu wale always wanahisi utapekua ukutane na wazee wa sins
 
Maisha yamekuwa magumu sana!wenye roho nyepesi ndo hao vibaka.
 
Huo ujinga sijaibiwa kwa hiyo style labda itumike nguvu simu ichukuliwe lakini eti naomba simu na mi nimpe big NO
 
Wanaibiwa kizembe sana unampa vipi simu mtu na humjui hadi anaondoka nayo unamuangalia tu. Huu ni uzembe uliopitiliza.
 
Weeeeh!!!
Wanakua wanaandika nini???
Aisee sijawahi kubahatika kusoma, ila kuna watu walishalizwa kiuzembe usikute ni dawa tu ya kukulevya na kupunguza uwezo wako wakufanya maamuzi, daftari ni njia ya kukuvuta karibu ili akuwekee hiyo dawa
 
Mimerudia kusoma mara 2 bado sijakuelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…