Jiji la Moshi mliwakosea nini Toyota Tanzania Ltd? Hakuna Branch wala Authorized Parts Dealer

Jiji la Moshi mliwakosea nini Toyota Tanzania Ltd? Hakuna Branch wala Authorized Parts Dealer

kayanda01

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
1,216
Reaction score
1,062
Moshi yote:

*Hakuna Toyota branch;

* Hakuna Authorized Dealer;

* Hakuna Authorized Service Workshop;

*Hakuna hata Authorized Parts Dealer

Nilisikiaga kuwa Moshi ni jiji, why Toyota Tanzania Ltd alipe kisogo jiji hilo la wajuaji?

Kuna jamaa zangu hapo wamefika mji huo jioni ya leo na kuhitaji service za magari yao, wameamua waghaili waende Arusha for services ndipo waendelee na safari.

Wanahitaji genuine Toyota parts, ila kila gereji wanayoelekezwa kwenda hapo Moshi mjini wanakuta ni zile workshops za 'Oil bei chee, oil filter tsh 5,000' 😁

Wakawauliza: Oil Filter og bei gani? Jamaa akawajibu: "Oil filter og Toyota ni Elfu 10 tu bwashee, sogezeni magari tuwape huduma za uhakika aisssee" 😂😂

Washkaji wamesepa Ara for cars' services! Moshi hamna kitu, pamejaa fake spare parts tu za kuua magari.
 
Mkuu, yawezekana kumbe Moshi bado ni Kijiji eeh?

Imagine mji mdogo wa Kahama kuna Toyota Authorized Dealer, lakini mji wa Moshi hakuna dealer!! [emoji16]
Kahama ni mji wa kibiashara zaidi unalishia mikoa kadhaa
 
Simply because Moshi hakuna wateja wakutosha au kutokana na ukaribu wa Moshi/Arusha branch iliyopo Arusha inatosha kuhudumia na Moshi
 
Nahisi RAJINDER MOTORS yupo vizuri. Yupo authorised na TOYOTA kukata na kuongeza chasis (refer landcruiser ndefu za utalii)
Wangeenda hapo RAJINDER MOTORS.
 
Moshi masikini, wenyeji wote wako huku Kimara sasa wamuwekee nani hilo duka?
 
Kwanza umedanganya huwezi kukosa spea ya gari mjini moshi ukaipata arusha
Haijawahi kutokea na haitawahi milele
 
Kahama ni mji wa kibiashara zaidi unalishia mikoa kadhaa

Upo sahihi Mkuu. Kahama ni mji wa kibiashara, na panapita high way road ya kimataifa kwenda nchi za jirani. Pale lazima Toyota aweke dealer.

Kinachoshangaza ni mji wa Moshi, pamoja na kuwa ndiyo makao makuu ya Mkoa Kilimanjaro, lakini hakuna hata dealer wa Toyota!
 
Simply because Moshi hakuna wateja wakutosha au kutokana na ukaribu wa Moshi/Arusha branch iliyopo Arusha inatosha kuhudumia na Moshi

Basi Toyota Tz Ltd hawaitendei haki Moshi. Huo mji ni mkubwa sana mkuu, magari ni mengi, na ndiyo makao makuu ya Mkoa Kilimanjaro. Kuna umuhimu wa kuwepo dealer pale.

Imagine mtu yupo Moshi, inamlazimu achome mafuta kwenda Arusha just kutafuta genuine Toyota spare parts!
 
Moshi siyo jiji mkuu, unaweza ukawa na point lakini umeandika kishabiki sana
 
Delership ya Toyota Spare and distribution kwa Moshi anayo Rajinder Motors, Kwa maelezo zaidi Mtafute Makonda alivolishika soko la Toyota cars.
 
Nahisi RAJINDER MOTORS yupo vizuri. Yupo authorised na TOYOTA kukata na kuongeza chasis (refer landcruiser ndefu za utalii)
Wangeenda hapo RAJINDER MOTORS.

Toyota alishakata dealership kwa Rajinder Motors muda mrefu sana tangu mwaka 2013.

Rajinder Motors is no longer an Authorized Toyota Dealer in Moshi town.
Toyota cuts ties with Moshi vehicle agent

IMG_20200821_093127.jpg
 
Back
Top Bottom