Jiji la Moshi mliwakosea nini Toyota Tanzania Ltd? Hakuna Branch wala Authorized Parts Dealer

Jiji la Moshi mliwakosea nini Toyota Tanzania Ltd? Hakuna Branch wala Authorized Parts Dealer

download.jpeg
download (1).jpeg
download (2).jpeg
Screenshot_20200821-093202.png
 
Moshi siyo jiji mkuu, unaweza ukawa na point lakini umeandika kishabiki sana

Achana na huo 'ushabiki' uliouona wewe mkuu. Basi jikite kwenye point/hoja ya uzi.
 
Mnaosema kuwa RAJINDER MOTORS ndiyo Toyota Authorized Dealer mjini Moshi, ni uongo!

Just mna dead information kuhusu hilo.
 
Boss pamoja na hayo yote lakini Rajinder is one of the few top garages in nation. Possibly top 3..

Hivi unafikiri kwanini Makonda alipeleka ile mikweche yote ya Polisi Tanzania nzima na ikatoka brand new ndani ya mwezi tu. Garage uweze kuunda Safari Cruiser na uize East Africa nzima then washindwe kununua genuine parts??

Acha masihara..
 
Kwanza umedanganya huwezi kukosa spea ya gari mjini moshi ukaipata arusha
Haijawahi kutokea na haitawahi milele

Hatuzungumzii just 'spea'.

Tunazungumzia 'genuine Toyota spea'.

Hapo Moshi, hakuna duka hata moja la spea ambalo ni Toyota Authorized. Halipo!!

Kama lipo, tutajie hapa.
 
Hakuna anayesema bado ni dealer mzee.. Ila hiyo tuzo ya best superdealer alishaishinda sana.

Alafu unafahamu kwanini aliporwa udealer?? Unafikiri ni hana vigezo?? Hivi angekuwa hana qualities za garage bora angepewa afanyie service magari yote ya Polisi Tanzania yale ambayo yalikuwa yamejifia na kubaki magofu kwenye vituo vya polisi.

Ugomvi na Toyota ni yeye kujiongeza kufunga coils na suspension za kampuni nyingine ambazo ni imara mara dufu kuzidi zile za Toyota. Na hii alikuwa akifanya kwa gari alizokuwa anaziunda kwa ajili ya pori (Safari Cruiser), na hapo ndio aliporwa udealer maana Toyota wao wanataka utumie spare parts zao tu na ingali kwa pori watu walikuwa wakizivunja sana gari zao.

Sasahivi hukuti gari yeyote ya porini inaenda service pale Toyota Arusha, zote zinafanywa na Rajinder Motors..
 
Ningekusaidia ila hoja yako iko kinafiki sana
Endelea kulima viazi kayanda

Wapi nimeandika nahitaji msaada wako?

Acha kuandika maneno ya kwenye kanga.

Mie nimeandika kwamba Moshi hakuna Toyota Dealer wala duka la spea ambalo ni Toyota Authorized. Hii ndiyo hoja ya uzi.

Wewe kama unaweza, prove me wrong kuhusu hilo.

Acha mboyoyo za kutaka kutoa msaada ilihali hujaombwa msaada wowote hapa.
 
Moshi yote:

*Hakuna Toyota branch;

* Hakuna Authorized Dealer;

* Hakuna Authorized Service Workshop;

*Hakuna hata Authorized Parts Dealer!!!!

Nilisikiaga kuwa Moshi ni jiji, why Toyota Tanzania Ltd alipe kisogo jiji hilo la wajuaji?

Kuna jamaa zangu hapo wamefika mji huo jioni ya leo na kuhitaji service za magari yao, wameamua waghaili waende Arusha for services ndipo waendelee na safari.

Wanahitaji genuine Toyota parts, ila kila gereji wanayoelekezwa kwenda hapo Moshi mjini wanakuta ni zile workshops za 'Oil bei chee, oil filter tsh 5,000' 😁

Wakawauliza: Oil Filter og bei gani? Jamaa akawajibu: "Oil filter og Toyota ni Elfu 10 tu bwashee, sogezeni magari tuwape huduma za uhakika aisssee" 😂😂

Washkaji wamesepa Ara for cars' services! Moshi hamna kitu, pamejaa fake spare parts tu za kuua magari.

Wapo ni Rajinder Motors wapo Majengo
 
Hatuzungumzii just 'spea'.

Tunazungumzia 'genuine Toyota spea'.

Hapo Moshi, hakuna duka hata moja la spea ambalo ni Toyota Authorized. Halipo!!

Kama lipo, tutajie hapa.
Aiseee, kutokuwa na duka lililo authorized haimaanishi eti mtu binafsi anashindwa nunua guniane parts na kuuza. Kwa Moshi na Arusha kupata guniane parts ni kama maji tu hapo Kenya boss..

Kuwa authorized ni tie za kibiashara zaidi kaka na unajifunga. Mchaga haishi hivyo sababu ya ujanja ujanja wake atataka auze spare parts 3 tofauti lakini za aina moja ili awe na wide range kwa mteja kuchagua atakayo afford.

Hilo ni jicho la kibiashara zaidi.. Na ndio maana Moshi ni Mji pekee ambao Tajiri wa kihindi havimbi kwa wazawa..
 
Nahisi RAJINDER MOTORS yupo vizuri. Yupo authorised na TOYOTA kukata na kuongeza chasis (refer landcruiser ndefu za utalii)
Wangeenda hapo RAJINDER MOTORS.
Toyota walishavunja ubia na Rajinder tangu 2013
 
Hakuna anayesema bado ni dealer mzee.. Ila hiyo tuzo ya best superdealer alishaishinda sana.

Alafu unafahamu kwanini aliporwa udealer?? Unafikiri ni hana vigezo?? Hivi angekuwa hana qualities za garage bora angepewa afanyie service magari yote ya Polisi Tanzania yale ambayo yalikuwa yamejifia na kubaki magofu kwenye vituo vya polisi.

Ugomvi na Toyota ni yeye kujiongeza kufunga coils na suspension za kampuni nyingine ambazo ni imara mara dufu kuzidi zile za Toyota. Na hii alikuwa akifanya kwa gari alizokuwa anaziunda kwa ajili ya pori (Safari Cruiser), na hapo ndio aliporwa udealer maana Toyota wao wanataka utumie spare parts zao tu na ingali kwa pori watu walikuwa wakizivunja sana gari zao.

Sasahivi hukuti gari yeyote ya porini inaenda service pale Toyota Arusha, zote zinafanywa na Rajinder Motors..

Mkuu, kwa hiyo sentence yako ya kwanza kabisa, umesomeka vyema kabisa, pamoja na hayo maelezo mengine.

So, kwasasa hapo Moshi, kuna Toyota Authorized Dealer yoyote?
 
Aiseee, kutokuwa na duka lililo authorized haimaanishi eti mtu binafsi anashindwa nunua guniane parts na kuuza. Kwa Moshi na Arusha kupata guniane parts ni kama maji tu hapo Kenya boss..

Kuwa authorized ni tie za kibiashara zaidi kaka na unajifunga. Mchaga haishi hivyo sababu ya ujanja ujanja wake atataka auze spare parts 3 tofauti lakini za aina moja ili awe na wide range kwa mteja kuchagua atakayo afford.

Hilo ni jicho la kibiashara zaidi.. Na ndio maana Moshi ni Mji pekee ambao Tajiri wa kihindi havimbi kwa wazawa..

Mkuu, nikiri kuwa unajibu hoja kimakini na una jicho la kibiashara. Nimekuelewa vyema kiongozi fisadi.
 
Back
Top Bottom