Jiji la Mwanza lawa kitovu cha Biashara ya Madini nchini

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,187



Likiwa jiji la pili kwa ukubwa nchini na wakazi wapatao 1,000,000 kwa sasa (700,000 mwaka 2012), Mwanza, maarufu kama Rock City, inatarajiwa kuanzisha Soko la Kimataifa la Madini, litakalowezesha kuratibu biashara ya madini hapa nchini.
Uwepo wa jiji hili katika Kanda ya Ziwa yenye utajiri mkubwa wa dhahabu na almas, ndio kichocheo kikubwa cha Jiji hili kuteuliwa ku-host Soko hilo. Madini ya Dhahabu (Geita) na almasi (Mwadui) yamekuwa yakichimbwa tangu kipindi cha ukoloni lakini pia yalichimbwa Mabuki (almasi) na Maganzo (dhahabu)
Hata hivyo, uchimbaji ulipanuka kwa kasi kubwa katika Awamu ya II ya Mkapa (2000s) ambapo uchimbaji wa dhahabu ulisambaa katika Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza hadi Mara, yakiwemo machimbo ya Bulyanhulu (ABG), Buzwagi (ABG) Tulawaka (GGM), Nzega (Golden Pride) Geita (GGM) Buhemba (ABG) North Mara (ABG), Buckreef, etc.
Kutokana na kudorora kwa kasi kubwa mwanzoni mwa 2010s kwa Sekta ya uvuvi ambayo ndiyo iliyokuwa chanzo cha Jiji hili kuwa mojawapo ya majiji yaliyokuwa yakikua kwa kasi barani Afrika miaka ya 1990s -2000s.
Uratibu wa Mwanza wa biashara ya madini nchini, utasababisha kuimarika kwa sekta ya usafirishaji hasa wa anga na hivyo kuneemesha Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kuanza polepole kupokea ndege za mashirika makubwa ya ndege duniani.
Vilevile, kwa kuwa Kituo hicho kimepangwa kuwa kwenye Rock City Mall, kutasaidia ku-boost sana biashara katika Mall hiyo kubwa sana hapa Afrika Mashariki.






 

Attachments

  • IMG_0800.JPG
    103.8 KB · Views: 122
  • IMG_0802.PNG
    246.2 KB · Views: 125
  • IMG_0804.JPG
    177.7 KB · Views: 118
  • IMG_0807.JPG
    131.8 KB · Views: 96
  • IMG_2787.JPG
    47.7 KB · Views: 128
Asante mkuu
Tanzania ni moja. Maendeleo ya Mwanza ni ya Moro, Dom, Mpanda,A town n.k.
Asili ya Watanzania ni umoja, upendo na mshikamano. Nafurahi kuwaona Wasukuma wakichungia Pwani, Sumbawanga n.k. Pia kuwaona Wamasai wakiuza dawa Kigoma, Kawe n.k. Bila kuvunja sheria.
Yote yatapita lakini Tanzania itaendelea kua moja kama ilivojengwa na wazee wetu.
 
Ni kweli mzee, Nchi hii ni yetu sote. Eneo lililojaliwa fursa lazima ziendelezwe eneo hilo. Ubaguzi ukifanywa na Serikali kwa kupendelea eneo fulani, ujue kiongozi atakayefuatia naye atafikiria upande wake.
Hata hivyo, hii Serikali ya sasa, inaangalia zaidi fursa za ndani za watu wa eneo husika na kuziendeleza.
 
Umesema vema mkuu
 
Nimependa...list iendelea Mbeya pawe kitovu cha mazao ya chakula wawekeze zaidi...Arusha kitovu cha utalii ,Dodoma mji mkuu,Dar mji muhimu wa biashara,Tanga warudishe heshima ya viwanda nk
mawazo mazuri
 
jambo hilo lilitakiwa lifanywe miaka mingi sana. Mwanza itakuwa haraka sana. angalia mfano Tel aviv Israel lilivyosoko la almasi dunia nzima...ni mipango tu.
 
na mererani,landanai, namalulu,winza zina hamishiwa mwanza.
 
Nimependa...list iendelea Mbeya pawe kitovu cha mazao ya chakula wawekeze zaidi...Arusha kitovu cha utalii ,Dodoma mji mkuu,Dar mji muhimu wa biashara,Tanga warudishe heshima ya viwanda nk
Yes naunga mkono hoja.
 
na mererani,landanai, namalulu,winza zina hamishiwa mwanza.
Na wewe mbona unaleta mawazo mgando hivyo? Mnapenda siasa majungu muda wote mnadhani mnamkomoa nani? Ni nani aliyeagiza kujengwa kwa ukuta wa Mererani ili uuzwaji wa Tanzanite ufanyikie hapo hapo Mererani?
Ulitaka dhahabu ambayo ndiyo inayoongoza katika sekta ya madini iletwe huko kwenu?
 
mda ninao kupumulia kisogoni ndio mawazo yangu huwa mgando. kuna mahali nimeongelea siasa? we katarina nn?
 
Jaman MUSOMA IWE KITOVU CHA UVUVI PIA
Wewe, hata kwa uvuvi, Mwanza inaishinda miji yote ya Tanzania na indeed yote ya Afrika Mashariki kwa kuwa iko katikati ya Kanda tatu maarufu za uvuvi Tanzania nzima -
  • Ukanda wa Kaskazini - Ukerewe (pamoja na Ukara na Irugwa)
  • Ukanda wa Magharibi - Kagera (Bukoba, Muleba na Bumbire) na Geita (Sengerema, Maisome, Kome na Chato)
  • Ukanda wa Mashariki - Mara (Rorya, Musoma, Mwibara, Bunda) na Simiyu (Busega na hata Magu).
Ukiangalia jinsi Mwanza ilivyo strategically kando ya Ziwa Victoria, utaelewa kwa nini Mwanza ndiyo imekuwa hub ya fishing industry muda wote hapa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…