Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Likiwa jiji la pili kwa ukubwa nchini na wakazi wapatao 1,000,000 kwa sasa (700,000 mwaka 2012), Mwanza, maarufu kama Rock City, inatarajiwa kuanzisha Soko la Kimataifa la Madini, litakalowezesha kuratibu biashara ya madini hapa nchini.
Uwepo wa jiji hili katika Kanda ya Ziwa yenye utajiri mkubwa wa dhahabu na almas, ndio kichocheo kikubwa cha Jiji hili kuteuliwa ku-host Soko hilo. Madini ya Dhahabu (Geita) na almasi (Mwadui) yamekuwa yakichimbwa tangu kipindi cha ukoloni lakini pia yalichimbwa Mabuki (almasi) na Maganzo (dhahabu)
Hata hivyo, uchimbaji ulipanuka kwa kasi kubwa katika Awamu ya II ya Mkapa (2000s) ambapo uchimbaji wa dhahabu ulisambaa katika Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza hadi Mara, yakiwemo machimbo ya Bulyanhulu (ABG), Buzwagi (ABG) Tulawaka (GGM), Nzega (Golden Pride) Geita (GGM) Buhemba (ABG) North Mara (ABG), Buckreef, etc.
Kutokana na kudorora kwa kasi kubwa mwanzoni mwa 2010s kwa Sekta ya uvuvi ambayo ndiyo iliyokuwa chanzo cha Jiji hili kuwa mojawapo ya majiji yaliyokuwa yakikua kwa kasi barani Afrika miaka ya 1990s -2000s.
Uratibu wa Mwanza wa biashara ya madini nchini, utasababisha kuimarika kwa sekta ya usafirishaji hasa wa anga na hivyo kuneemesha Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kuanza polepole kupokea ndege za mashirika makubwa ya ndege duniani.
Vilevile, kwa kuwa Kituo hicho kimepangwa kuwa kwenye Rock City Mall, kutasaidia ku-boost sana biashara katika Mall hiyo kubwa sana hapa Afrika Mashariki.