Jiji la Nairobi lafungwa, polisi watanda kila kona

Jiji la Nairobi lafungwa, polisi watanda kila kona

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014

Wakati Watanzania wakiadhimisha siku ya Sabasaba ikiwa ni maadhimisho ya kimataifa ya Biashara, kwa Wakenya siku hiyo inakumbukwa kuwa ni ya kiharakati, ikienda hadi miaka 1990 ambapo baadhi ya wanasiasa walifanya mkutano wa kihistoria katika uwanja wa Kamkunji jijini Nairobi, kushinikiza mabadiliko ya Katiba mpya kuruhusu kuwepo kwa vyama vingi.

Serikali ya wakati huo ya chama kimoja cha KANU ikiongozwa na Rais Daniel Arap Moi, ilikataa kutoa kibali cha kufanyika kwa mkutano huo, lakini wanaharakati na wanasiasa hao wakiongozwa na Charles Rubia, Martin Shikuku, Raila Odinga, Gitobu Imanyara, Jaramogi Oginga Odinga na wengine waliendelea na mkutano huo kwa nguvu.

Vurugu zilizuka jijini Nairobi kwa siku nne na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20 kupoteza maisha na zaidi ya wengine 1,000 kukamatwa.

Baada ya Shinikizo hizo, rais wa wakati huo Daniel Arap Moi alikubali kuwepo kwa vyama vingi.

Kwa siku ya leo ilitarajiwa kuwe na mwendelezo wa maandamano nchini humo yanayoratibiwa na vijana maarufu GEN-Z, lakini leo wamekwama kuingia katikati ya jiji, kwani polisi wa nchi hiyo wamefunga barabara zote kuu na kuufanya mji huo kuwa kimya.
 
Katiba mpya imeleta matunda ya maandamano
 
Maandamano ni haki.. ukikuta wananchi wa nchi fulani hawafanyi maandamano ja hao ni WAFU! na misukule
Swali.
Watz hawafanyi maandamano kwa sababu wameridhhika, yanakazwa au hawajui haki zao?..
Ulishawahi kuona maandamano Vatican?
 
Ulishawahi kuona maandamano Vatican?
Vatikani kuna
Uhaba wa dawa?
Watu wanasusa maiti kwa kukosa pesa kama muhimbili
Maji yanakatika?
Umeme je?
Hakuna ajira kwa vijana?
Barabara zao mbòvu?
Watu wanatekwa na kuuwawa hovyo?
Wanafunzi wanakaa chini shuleni?
 
Kumbe wameanza sikumingi tuu.
Wacha waendelee kukamuana maana ishawaingia kwenye damu
 
Ulishawahi kuona maandamano Vatican?
Unakakari sana ndugu yangu. Vatican ni unique case. Hata hivyo maandamanona migomo Italy vipo kwa wingi usivyotegemea. Unajua kama hujawahi kuishi Ulaya huwezi kujua jinsi hizi nchi zilivyo na migomo au maandamano kwa wingi. Utadhani wako kimya na hawana conflict na watawala kabisa.
 
Back
Top Bottom