Jiji la New York lilikumbwa na mvua kubwa na radi Alhamisi jioni Agosti 20, 2026, hali iliyosababisha mafuriko ya ghafla na kugeuza baadhi ya barabara kuwa kama mito. Mji wa Queens ilikuwa miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi, huku magari yakizama kwenye maji na wasafiri wakilazimika kutembea kwenye maji yaliyofika magotini.
Mamlaka ya Usimamizi wa Dharura (NYC Emergency Management) ilitoa tahadhari ya usafiri baada ya jiji kuwekwa katika kiwango cha wastani cha hatari ya mvua kubwa. Zaidi ya watu milioni 25 kaskazini-mashariki mwa Marekani waliwekwa chini ya tahadhari ya mafuriko, huku huduma za Amtrak kati ya Albany na New York zikisitishwa kutokana na maji kwenye reli.
Mafuriko hayo yameibua tena mjadala kuhusu mfumo wa majitaka na mifereji ya maji ya mji wa New York, ambao umekuwa ukikosolewa kwa kushindwa kukabiliana na mvua kubwa. Mamlaka za Jiji zimeahidi kuwekeza mabilioni ya dola kuboresha miundombinu hiyo, lakini matukio ya mara kwa mara yanaendelea kuibua maswali
Soma Mafuriko yalivyokumba Jiji la New York, miundombinu ya mifereji yazidiwa barabara zafurika maji