El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 297
- 537
Najua kwa hakika kabisa kwamba, kupanda hadhi kwa maeneo, mfano mji kuwa manispaa na manispaa kuwa Jiji Kuna vigezo vyake.
Mfano , idadi ya watu, Pato la eneo husika, na sababu nyingine nyingi za kisiasa ambazo sijui kwa hakika zinaingiaje kwenye kupandisha eneo hadhi.
Sababu zao zinaweza kuwa sawa ndiyo, lakini Kuna jambo muhimu ambalo linasahulika sana, nalo ni miundo mbinu ya barabara.
.Napendekeza miundo mbinu Bora hasa ya barabara iwe kigezo Cha kupandisha hadhi eneo Fulani.
Tembelea miji na majiji ya nchi yetu ndo utaona maajabu.
Hakuna kabisa barabara za maana mara tu unapotoka eneo la katikati ya miji, manispaa na majiji yetu.
Tanga, Geita mji, musoma, walau unaweza sema ni maeneo yenye hadhi hiyo iliyonayo.
Majiji yetu ndo kabisaaaa, mbeya barabara nje kidogo ya CBD ni mashimo matupu na hazivutii, Nenda mwanza nje ya CBD. Arusha ndo kabisaaa, ukitoka tu nje ya CBD hutamani lile eneo kuitwa Jiji. Miundo mbinu ya barabara ni mibovu than ever before. Ni matope na makorongo matupu.
Mpaka inafika mahali unajiuliza hivi viongozi hupita kweli barabara na hasa viungani?
Inawezekanaje baada tu ya kuvuka maeneo ya katikati ya miji huoni tena sura ya kuitwa Jiji?
Barabara zilizoko maeneo mengi ni chafu, mashimo na hazipitiki kirahisi na vyombo vya usafiri.
Hivi wakubwa zetu hawajui kwamba , idadi kubwa ya watu unatokea hayo maeneo ambayo hayapewi miundo mbinu Bora?
Tunarahisishaje shughuli za uchumi na kupunguza gharama kwa watu wetu kama barabara zimejaa makorongo vile.
Vipi watu wetu wanaokoa muda au wanapoteza muda kwenye mashimo yanayoitwa barabara?
Vipi kijamii tunasaidia watu wetu kuishi kisasa na kwa ustaarabu?
Ebu nenda uone maeneo yenye hadhi mbovu ya barabara yalivyojaa nyumba za mabanda mabanda yanayofanya hata miji yetu kuwa michafu. Nenda uone maeneo yenye barabara mbaya yalivyojaa wavuta bangi na wanywaji wa pombe za kienyeji!
Hapa suala la kimantiki tu kwamba" mahali ambako hakuna barabara za kupendeza, wastaarabu hawaendi kujenga na kuishi huko as a result wataishi tu watu wa hali duni na kwa maana hiyo, maeneo hayo yatakuwa duni na yatajenga taswira duni ndani ya watu nao watakuwa duni. You are what you see"
Niwaombe viongozi wetu, kwa Leo niwasemee wakuubwa mikoa ambayo ni majiji, Dar, Dodoma, Mwanza, Mbeya , Arusha , na of course Tanga, kuyapa hadhi majiji haya kwa kujenga barabara zenye hadhi ya majiji. Vinginevyo majiji yatakuwa vijiji.