Jiko la gesi lilivyozima ndoto na uhai wa Familia ya Abedi Falhum Msangi

Mmmmmhhhhhhh uzi unatufundisha lakini pia unaogofya.... Mola Mlezi amfanyie wepesi aliyebaki ili kuihuisha familia yake....

Gesi kwa hakika ni mtihani hasa kwa familia zenye watoto ambao kimsingi upends kujifunza na kujaribu
 
Hii stori kuna vitu havijakaa sawa. Huwezi kuwa umezingirwa na moto halafu uwe macho unaingia na kutoka.

Mtu aliyeungua kiasi hicho hawezi kuongea na kukupa stori namna hii.
Omba yasikukute.

Angeweza kuwa na roho ya kutokujali akawaacha hao wengine watatu ndani leo hii angekuwa hai but kama binadamu akiwaza ndani kuna mtoto ni damu yake kuna mke wake huyo h/girl unaweza kusema angeachana nae ila kwa utu na kama mwanaume unajiona unaweza kupambana.yapo mazingira yanamkuta mtu hata huo moto hausikii.

Mungu awahifadhi salama hao marehemu.
 
Kosa namba waliacha gas itoke kwanza ndipo wakawasha hii ni hatari sana gasi inakuwa ishasambaa nyumba nzima so ukiwasha tu kiberiti nyumba yote inalipuka.
Inatakiwa uwashe kwanza kiberiti ndipo uwashe gas
Hili ndio kosa wengi hawalijui kutumia ile mitungi midogo

Washa kwanza kiberiti ndio ufungue gesi

Otheriwise mtakufa huku mnaona
 
Unapiga kama vile ulikuwepo.

Mtu mzima anaeleta uzi wa maafa wewe unadhani chai

Mpaka yakutokee ndio utaelewa.

Wazee wa chai mnakera ssna kila kitu kwenu ni chai.

Mna,ingua
 
Sawasawa mkuu. Pole nyingi kwa wafiwa.
 
Unapiga kama vile ulikuwepo.

Mtu mzima anaeleta uzi wa maafa wewe unadhani chai

Mpaka yakutokee ndio utaelewa.

Wazee wa chai mnakera ssna kila kitu kwenu ni chai.

Mna,ingua
Habari yenyewe sio ya uongo. Uwasilishaji wake ndio una mashaka kiasi kikubwa.
 
[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
 
Abeid,Classmate wangu 2013-2016. Mwenyezi Mungu ampe yeye na familia yake pumziko la amani.
 
Aisee ni story inahuzunisha sna lakini pia umetoa elimu nzuri sna
 
Ref. John Walker pia alikufa kwa kulipukiwa na jiko la gesi.
 

Hii stori imenisisimua sana. Siku kama tano zilizopita nilijisahau nikaacha gesi inatoka, wife alivyoingia akahisi harufu. Akafunga jiko vzr na kufungua milango na madirisha na sisi tukatoka nje. Nilijisikia vibaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…