Uchaguzi 2020 Jimbo gumu kupata mwakilishi ni Kawe

Uchaguzi 2020 Jimbo gumu kupata mwakilishi ni Kawe

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2015
Posts
2,805
Reaction score
3,640
Hili jimbo kwa ujumla ni gumu kupata mwakilishi sahihi kwa upande wa Chama chetu Tawala.

Ni jimbo liko mjini, lina wapiga kura wataalazi sababu ya literacy level iko juu, na linachangamoto nyingi za barabara, mifereji, wingi wa wanafunzi, wingi wa bodaboda, wafanyabiashara ndogondogo na walipakodi wengine kwa ujumla

Watia nia mpaka sasa kwa stori za town wamefika watu 32.

Kwa waliosikika Paskali, Timothy, Furaha, Gwajima, Yusuphu Mwenda, Emmmanuel Mbasha, Kipi,

Kwa kweli kamati ya kuchuja itabidi ije na vigezo vingi ili kutuletea Mgombea atakayeshindana na Upinzani.
 
Watu wa Lumumba mna mambo nyie!!! Mpeni jimbo Gwajima maana Tanganyika pekazi inampa shida kuirudisha mikononi mwake.
Mkuu hiyo ndiyo habari ya mujini, yaani kapigwa stop kabisa na huyo kidume mtarajiwa kujihusisha na siasa.
 
Halima kafanya kipi cha kumfanya aendelee.
Kama serikali inayo kusanya kodi iliacha kutimiza wajibu wake ili waseme Halima hakufanya kitu sasa ni muda muafaka kwa wapiga kura kumpa tena Halima ili kuitia adabu CCM na serikali yake kwa mateso iliyo wapa wakipa kodi wa Kawe.

Msituletee siasa za kishamba hapa. Halima hakuwa na serikali ila alijitahidi sana kuwa tetea wananchi wa Kawe

Tuna sema tano tena kwa Halima
 
CCM mnajua kabisa kwamba ni kwa mtaji wa wajinga tu ndio mnapata kura ndio maana majimbo ya maeneo ya watu wenye akili nzuri mnapata shida sana. Dar, Kili, Arusha, Mbeya, Mara..
 
Kazi rahisi sana tumieni tu polisi na wale makada wa CCM Wakurugenzi na tume kwa pembeni lengo lenu litakuwa limetimia
 
Kawe ni jimbo gumu kweli. Ni suala la CCM kupanga karata na kuweka anayekubalika na wengi, hapa utakutana na mwana kwao Kippi Warioba, angalau anaweza kusimama na kueleweka kwa wapiga kura.

Anajua kujenga hoja na hana bla blaa za wanasiasa wengi.
 
Halima kafanya kipi cha kumfanya aendelee.
Mkuu watu wote wenye elimu zao wanajua majukumu ya mbunge,Ila vilaza Kama ninyi ndo mnadhani kazi ya mbunge ni kujenga barabara,kuzibua mitaro ya maji machafu na kuwapa lift
 
Mkuu hiyo ndiyo habari ya mujini, yaani kapigwa stop kabisa na huyo kidume mtarajiwa kujihusisha na siasa.
Tunasikia anategemea kuolewa ili awe mama wa nyumbani, amechoka kuwa single na mume wake mtarajiwa kampiga stop siasa.
Hiyo taarifa waambie wana Lumumba wenzio wanaosemaga humu kuwa Halima ni lesbian.
 
tatizo sio watu wanaojielewa,je waliojiandikisha kupiga kura ni watu wa aina ganii?? mda wa kujiandikisha wasomi walikuwa bize na mda wa kufanya maamuzi wasomi wanalalamika....
 
Mkuu uchaguzi wa mwaka huu kuna mtindo mpya wa wengi wanataka faili zao zipite tu. Mwenyekiti sisiemu awateue kwa kazi zingine mbeleni.
 
Back
Top Bottom